Mwenyekiti
wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Adam
Kimbisa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge
hilo, Mh. Shy-Rose Bhanji, mbunge wa bunge hilo, Mh. Nderakindo Kessy na
kulia ni Mhe. Makongoro Nyerere.
Katibu
wa wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mhe. Nderakindo Kessy na Mwenyekiti wa wabunge wa
Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Adam Kimbisa.
Nasisitiza.....
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania wakibadilisha
mawazo baada ya mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka
Tanzania,Mh. Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti, Mh. Adam Kimbisa, Mh.
Nderakindo Kessy na Mh. Makongoro Nyerere.
Mbunge
la Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. Makongoro Nyerere
akipeana mkono na Katibu wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe.
Shy-Rose Bhanji.
Na.Habari Mseto Blog.
Bunge
la tatu EALA limeridhia Tanzania kupata kikao chake rasmi ambapo sasa
kikao kitafanyika Dodoma na vikao vingine viwili kufanyika Arusha ambayo
ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti
wa wabunge wa Tanzania, mhe. Adam Kimbisa amesema hayo katika mkutano
na wabunge watanzania EALA, na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
leo.
Mhe.
Kimbisa amesema katika ratiba ya vikao vya Bunge la EALA, Tanzania pia
imepata rasmi kikao kimoja ambapo sasa kitafanyika mjini Dodoma.
Vile vile amesema kikao hicho kinaweza kufanyika Dar es Salaama au Zanzibar.
Amefafanua
kwamba, Bunge limeridhia vikao viwili vifanyike Arusha, kimoja
kifanyike Tanzania sambamba na nchi zingine wanachama; Kenya, Uganda,
Rwanda na Burundi kupata kikao kimoja kila nchi kwa mzunguko.
Amesema
nchi ambayo itakosa kikao kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014, ndio
itakuwa nchi ya kwanza kupata kikao cha mwaka ujao wa fedha.
Hata
hivyo amesema, vikao vikao viwili vya Arusha vitakuwa ni vikao vya
bajeti na ukaguzi wa mahesabu ambavyo ni vikao muhimu sana katika Bunge.
Mhe.
Kimbisa amesema kikubwa wananchi wanachotakiwa kufahamu ni kuwa
linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha ni Makao Makuu
na kwamba haiko Tanzania kwani nchi zote tano ni wadau wa Arusha.
Naye
Katibu wa watanzania,Mh. Shy-Rose Bhanji amesema ni jambo la kujivunia
kwamba Tanzania sasa itakuwa na kikao rasmi kwa njia ya mazungumzo. Hii
ni hatua nzuri vile wananchi pia watapata mwamko wa masuala
yanayojadiliwa Bungeni.
Hatua
ya maridhiano hayo imefuatia mgoghoro ulioibuka miongoni mwa wabunge wa
EALA kwamba vikao vya Bunge hilo vifanyike Arusha kwa mwaka mmoja wa
fedha na si kwa mzunguko kama ilivyozoeleka kuanzia Bunge la pili.
Wabunge wengi isipokuwa watanzania walitaka vikao viendelee kwa mzunguko nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Arusha.
Vikao
vya EALA hadi mwaka wa fedha June 2012/June 2013 vilikuwa vitano kwa
mwaka. Vikao hivyo vimeongezeka kuwa sita. Vikao hufanyika kila baada ya
takriban miezi miwili, kwa kipindi cha wiki mbili.
No comments:
Post a Comment