Na Waandishi wetu, Mwananchi
(email the author)
Kwa ufupi
- Mabosi huwatafutia safari kama njia ya kuwanasa kwa kuwa wanapokuwa hotelini pekee, wanawake wengi wanakosa ujasili wa kukataa.
- Wengine hutoa ofa kama vile kupandishwa vyeo, kununulia magari au hata safari za nje.Wengi wanaofanya haya ni waume za watu, wengine ukitajiwa ni ngumu kuamini kwa namna wanavyoonekana wana hekima usoni au mavazi yao.
Licha ya harakati mbalimbali za kumkomboa
mwanamke, bado kuna mabosi nchini wanawanyanyasa wanawake kwa
kuwalazimisha kufanya nao ngono.
Wapo wanaonyanyaswa au hata kuteswa ikiwemo
kusemwa maneno machafu au kutishiwa kufukuzwa kazi kwa sababu tu
wamekataa kutoa penzi kwa bosi.
Wale wanaokubali, wengine wanaishia kupewa ahadi
hewa za kufundishwa magari, kupelekewa kozi mbalimbali. Hata hivyo mbaya
zaidi ni kwamba mabosi wengine hata kama wameoa, hupenda kuwamiliki
wanawake hao kana kwamba ni wake zao kwa kuwafuatilia sana nyendo zao.
Ukahaba wa mabosi hufanywaje?
Baadhi ya wanaume kwa mwonekano ni vigumu kuamini
kama ndiyo wanaofanya vitendo vichafu kwa wafanyakazi wao. Wanaposimama
kwenye vikao, utasema mtu huyu, lakini wafanyakazi wa kike wamekuwa ni
wenye kuwanyanyasa mno.
Baadhi ya mabosi wamekuwa wakitoa vitisho kuwa
‘kama hunipi penzi nitakuporomosha cheo au hata kukufanyia visa vyovyote
hadi uhame’.
Katika baadhi ya ofisi badala ya mabosi kutumika
kama washauri wa wafanyakazi wao kuzipenda ndoa na nyumba zao, ndio
wamekuwa wakitumia fedha zao kuwahonga wanawake hata magari, huku
makatibu muhtasi wakidaiwa kuwa ndio wanaosumbuliwa zaidi.
Wapo mabosi huwaingia wanawake wakiwemo wake za
watu kwa kuwapangia safari za mikoani au nje ya nchi hasa wanapoona
hawana wepesi wa kukubaliana na matakwa yao.
“Nakumbuka kuna bosi mmoja katika ofisi moja nyeti
aliwahi kudaiwa kumnunulia gari mke wa mtu kabla ya kuhama chombo
hicho,” anasema mkazi mmoja wa Kimara.
Bosi aliweza kumpa safari ya nje mwanamke na kisha kumnunulia gari zuri kuliko la mumewe.
Hii ni moja ya kati ya matukio mengi ya mabosi
kuwaingiza wafanyakazi wao katika ngono badala ya kuwa ndio washauri
wema kwa wafanyakazi ili waweze kuziheshimu ndoa zao.
No comments:
Post a Comment