Wednesday 15 April 2015

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI MTEMBELEA MZEE SAMWEL RWANGISA NEW YORK MAREKANI KUMJULIA HALI YA AFYA YAKE.

 Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki amemtembelea Mwanasiasa mkonge katika Taifa hili la Tanzania Mzee Samwel Ntambala Rwangisa nyumbani kwake New York Marekani kumjulia hali ya afya yake,Mzee Rwangisa yuko nchini marekani kwa matibabu ya afya yake takribani miezi mitano sasa.(katika picha Kushoto ni Mzee Rwangisa, Murungi kichwabuta na Balozi Kagasheki)wakiwa nyumbani kwa mzee Rwangisa New york Marekani.
 Mzee Rwangisa akiongea na wananchi  kwa njia ya simu akiwa New York Marekani kupitia redio Kasibante 88.5 ya Mjini Bukoba, Kikubwa amewaomba wananchi kuwa wamoja na shikamano.
 Akiongea na Redio Kasibante.
 Balozi Kagasheki akiongea na Redio Kasibante akiwa New York Marekani  akimshukuru Mkuu wa wilaya  ya Bukoba  kwa namna anavyoshughulikia tatizo la chakula kwa shule za sekondari zilizofungwa, pia amelipongeza jeshi la polisi linavyoendelea na jitihada za kuhakikisha hali ya usalama kwa wananchi jimboni.
 Mh Murungi Kichwabuta (Diwani viti maalumu) akiongea na redio Kasibante akiwa New york Marekani , ameelezea maendeleo ya hali ya afya ya baba yake mzee Rwangisa, pia amewataka wanawake kuwa na mshikamano na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
 Katikati ni binti mkubwa wa Balozi Kagasheki anaeishi Marekani Tausi Kagasheki.
Jamcobukoba.blogspot.com inakutakia afya njema mzee Rwangisa, picha hizi kwa hisani ya Bi Tausi Kagasheki kutoka Marekani.

No comments:

Post a Comment