- Mshindi wa droo ya tano wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Furaha Kitigi akishuka kutoka kukagua Bajaji aliyokabidhiwa na Meneja Usambazaji wa Bidhaa kutoka Tigo Bw. Suleiman Bushangama (kulia) katika hafla iliyofanyika Tandika sokoni, Dar es Salaam.
- Mshindi wa droo ya tano wa promosheni yaTigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Furaha Kitigi akipungia kutoka kwenye Bajaji yake mpya kabisa mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Usambazaji wa Bidhaa kutoka Tigo Bw. Suleiman Bushangama (kulia) katika hafla iliyofanyika Tandika sokoni, Dar es Salaam.
Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa droo ya tano wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bi. Happiness Simon katika hafla iliyofanyika Tandika sokoni, Dar es Salaam
Mshindi wa droo ya tano wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bi. Happiness Simon akionyeshea ufunguo wake wa Bajaji mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000 aliyokabidhiwa katika hafla iliyofanyika Tandika sokoni, Dar es Salaam. Akishuhudia ni Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif
MAMA TUNU PINDA AZINDUA MRADI WA KUSAIDIA WATOTO KIKE NCHINI
Mgeni rasimi Mama
Tunu Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya kumsadia mtoto
wakike kushoto kwake ni mkururugenzi
Mtendaji wa Tmarc Bibi Diana Kisaka ambao ndio wandaji wa mradi huo kulia kwa mama pinda ni Ludovicka Tarimo mshauri wa maswala ya
jinsia kutoka USAID anayefuatia ni Mkuu wa voda com Foundation Bwana Yessaya Mwakifulefule sherehe hizo
zimefanyika mkoani Mtwara picha na Chris Mfinanga
Mama Tunu Pinda naonekana akicheza ngoma marufu ya kimakonde ambayo ilikuwa ikiburusha wageni katika uzinduzi wa mradi wakumsaidia mtoto wa kike
Meneja wa voda com foundation Bwana Mwakifurefure akiwahutubia wageni walikwa voda com wamehusika katika kuweza mradi huo ambawalichangia kiasi cha shilingi milioni miamoja sitini picha na Chris Mfinanga
Mama Tunu Pinda naonekana akicheza ngoma marufu ya kimakonde ambayo ilikuwa ikiburusha wageni katika uzinduzi wa mradi wakumsaidia mtoto wa kike
Meneja wa voda com foundation Bwana Mwakifurefure akiwahutubia wageni walikwa voda com wamehusika katika kuweza mradi huo ambawalichangia kiasi cha shilingi milioni miamoja sitini picha na Chris Mfinanga
HUU NI WIZI MTUPU
Mfanyakazi
wa Inayojiita kampuni ya kukusanya Ushuru ya MTAA WA OYSTERBAY BEACH
PARKING, ambaye hakutaka kutaja jina lake akiandika risiti ya ushuru wa
maegesho ili kuweka katika moja ya gari lililokuwa katika ufukwe wa Coco
Beach, ili alipwe ushuru wa maegesho hayo kiasi cha Sh. 1000 kila gari.
Mfanyakazi huyo alipohojiwa na mtandao huu alisema kuwa anauwezo wa
kukusanya hadi magari 20 kwa siku jambo ambalo si la kweli kwani kwa
muda mchache tu alishapitia magari zaidi ya hayo.
Na
alipoulizwa zinapopelekwa fedha hizo baada ya kukusanywa alisema ''Mimi
sijui zinapopelekwa kwani mimi ni mfanyakazi tu na nikishakusanya
nampelekea Bosi ndo anajua zinapokwenda, kwa siku naweza kukusanya
ushuru hadi wa magari kama 15 hivi,kwa sababu sipo peke yangu tupo wengi
katika eneo hili lote''. alisema mfanyakazi huyo.
Hata
hivyo baadhi ya watu waliokuwapo ufukweni hapo, walisikika wakin'gaka
kutoa ushuru huo, huku wakimhoji ''Tutoe ushuru wa Parking kwa lipi,
hata usafi tu hamfanyi nyie mnajua kuchukua hela tu, na kwanza
mlishazuiliwa kukusanya pesa hizi bado tu mnaendelea na wizi wenu''.
alisikika akilalama jamaa mmoja
Imeelezwa
kuwa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kukusanya ushuru huo,
ilishawahi kuwa na mgogoro kipindi cha nyuma, ambapo wahusika waliwahi
kukamatwa na kufikishwa hadi Kituo cha Polisi na kuzuiliwa kufanya kazi
hiyo, kutokana na kutokuwa na ruhusa ya kufanya hivyo na kwamba
hawatambuliki na Halmashauri wala serikali, lakini wanaendelea kinyemela
na kufanya baadhi ya watu wanaowafahamu kuwagomea kutoa ushuru huo
wanapofuatwa kulipia parking hiyo.
Na
hata ukiitazama kwa makini Risiti hii haionyeshi Adress kamili ya
wahusika, haina mhuri wala namba za simu zaidi ya kuandika jina la
Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Beach, Sasa kuna kila haja ya kuwahoji
Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo ili kujua Mapato na Matumizi ya
ukusanyaji wa Ushuru huu, unaokusanywa kuanzia Jumatatu hadi Jumapili
bila kupumzika na zinapokwenda Fedha hizo.
Hii
ndiyo Risiti yenyewe inayotolewa baada ya kutoa Sh. 1000 kwa
mkusanyaji, ambaye pia anakuwa ameambatana na vijana wawili waliovalia
kiraia Jinzi na Tisheti na makofia ya Sweta, wakimlinda mkusanyaji huyu
mdada na kupiga mkwara kwa anayeonekana kukaidi kutoa Buku.
Mkusanyaji
akiandika Risiti hiyo, ambayo hata akiisha ichana haibaki Kopi yake
kuonyesha kilichoandikwa, Yaani ni Vishina kwa kwenda mbele.
Akienda kuweka risiti katika gari
Akitimiza wajibu wake kuweka katika gari....
Huyu ndiye mkusanyaji wa ushuru katika Fukwe hiyo.
No comments:
Post a Comment