Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akitoa
risala yake kwenye hafla ya kukabidhi Taa 200 za Nishati ya Jua kwa
Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande ikiwa ni mwendelezo ya
kampeni iliyozinduliwa na Hoteli ya DoubleTree By Hilton jijini Dar kwa
wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza hoteli hiyo kwa kubuni
kampeni kama hiyo kwani Taa hizo ni rafiki wa mazingira kwa kuwa
zinatumia Nishati ya Jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao
pia kupata Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme na pia
itaongeza ufaulu kwa Wanafunzi kwa sababu watakuwa wanauwezo wa
kujisomea nyakati za usiku.
Aidha
amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo
yaliyokusudiwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack
Vinivuni na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton
Rode Perk pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by
Hilton Florenso Kirambata (wa pili kulia).
Mkurugenzi
wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata
(katikati) akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia taa ndogo za mezani
zinazotumia Nishati ya Jua na umuhimu wake tofauti na kutumia Mafuta ya
Taa kwa Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Mji Mpya
wakati uongozi wa hoteli hiyo ulipotembelea shule hiyo iliyopo
Mabwepande kwa nia ya kuendesha mafunzo na kugawa Taa 200 bure kwa
Wanafunzi hao. Kushoto ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Mh. Angellah Kairuki (Mb) na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double
Tree by Hilton Rode Perk.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb)
akikabidhi rasmi Taa hizo kwa mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mji
Mpya iliyopo Mabwepande leo jijini Dar. Katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo
wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata na Kulia ni
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
Mwenyekiti
wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni akitoa shukrani kwa uongozi wa
hoteli ya Double Tree by Hilton kwa kuwa na mkakati madhubuti wa
kuwaelimisha vijana umuhimu wa matumizi ya Umeme mbadala wa Nishati ya
Jua ambao ni rafiki wa mazingira.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Mji Mpya Davis Mkaruka akizungumza baada ya
mafunzo yaliyolewa na Double Tree by Hilton kwa wanafunzi wa darasa la
saba akisema ilikuwa ni njia nzuri ya kuwaelimisha watoto juu ya nishati
ya jua na kuwa wamefurahi kupewa bure taa ndogo za mezani ambazo ni
rahisi kutumia na zina faida nyingi kwao na familia zao.
Wanafunzo
hao wakifurahia Taa ndogo la ‘Solar Energy’ walizopewa. Nyuma ni Bw.
Florenso Kirambata na Meneja Mkuu wa hoteli ya Double Tree by Hilton
Hotel Rode Perk.
Hoteli
ya Double Tree by Hilton Dar es Salaam leo imefanya ziara katika Shule
ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande kwa lengo la kuendesha mafunzo kwa
wanafunzi wa darasa la saba kuhusu umuhimu wa umeme wa nishati ya jua.
Mafunzo
hayo ni sehemu ya mkakati wa Double Tree by Hilton wa miaka miwili wa
kuwakufahamisha na kuwashirikisha wanafunzi juu ya faida za nishati ya
jua tofauti na matumizi ya mafuta ya taa, kuni na vyanzo vingine vya
mwanga ambavyo vina madhara kwa mazingira, afya na vifaa vya nyumbani.
Katika
ziara hiyo shule hapo Hoteli ya Double Tree by Hiltonimegawa kwa
wanafunzi hao taa ndogo za mezani 200 zinazotumia nishati ya jua, ambazo
wanafunzi hao wamekwenda nazo majumbani kwao kuzitumia kusomea usiku
kwa faida yao na familia yao.
No comments:
Post a Comment