Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jinsi
waandaaji wa vipindi wanavyoweza kutafuta habari nzuri zenye kuelimisha
kwa ajili ya redio za jamii na pia mbinu wanazoweza kutumia ili
kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
Akizungumza katika warsha ya siku nne
inayoshirikisha waandishi na maripota wa redio za jamii inayofanyika
Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Bi. Ledama ameongeza kuwa upo umuhimu
wa kuwajengea uweze watendaji katika redio hizo ikiwemo kuwafundisha
namna ya kutumia mtandao wa Intaneti kwa ajili ya kuboresha uandishi na
utangazaji , haswa katika maeneo muhimu yanayoigusa jamii ikiwemo Elimu,
Afya na Kilimo na pia jinsi redio hizo zinavyoweza kuandaa vipindi
vitakavyoigusa jamii moja kwa moja.
Kwa jumla warsha hiyo ya siku nne kwa
waandishi wa habari wa redio za jamii imeangalia kwa mapana mambo muhimu
ya kijamii, na kuchambua mambo hayo ni yapi ambapo imegusia masuala ya
Afya na Kilimo pamoja na mambo mengine na kuangali fursa zinazopatikana,
pia changamoto zinazokabili masuala hayo na kutathmini nini kifanyike
ili kuboresha utendaji na utoaji huduma katika sekta hizo.
Mtaalam wa Kilimo kutoka Idara ya
Kilimo wilayani Sengerema Bw. Joseph Manota akizungumza katika warsha ya
waandishi wa habari wa redio za jamii inayofanyika mkoani Mwanza ambapo
fursa zinazopatikana katika sekta ya Kilimo na jinsi ya kuzitumia ili
kufanikisha sera ya Serikali ya Kilimo Kwanza na pia amezungumzia
changamoto zilizopo katika kutimiza sera hiyo na namna gani maafisa wa
Kilimo pamoja na Serikali kwa ujumla wanaweza wakafanya kukabiliana nazo
ili kutimiza malengo ya kukuza Kilimo.
Mshauri wa redio za jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Pichani juu na chini ni waandishi na
maripota wa redio za jamii wanaohurudhuria mafunzo hayo yanayofanyika
kwenyen kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Wilayani
Sengerema mkoani Mwanza.
Mwezeshaji kutoka Kitengo cha Habari
cha Umoja wa Mtaifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha baadhi ya
machapisho ya Umoja wa Mataifa ambayo yatawasaidia katika kuandika
habari zao kiufasaha.
Mmoja wa watangazaji wa Redio Kahama
FM William Bundala (Kijukuu cha Bibi K) akitoa mrejesho wa mafunzo
yaliyopita ambayo yameleta mabadiliko makubwa kwa kituo chao kwa Mshauri
wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu
Afisa Elimu, Takwimu na Vifaa wilaya
ya Sengerema mkoani Mwanza Pius Lwamimi akizungumza na waandishi wa
habari na maripota wa redio za jamii nchini ambapo aligusia changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta Elimu wilayani humo na kuwaasa kutumia
redio zao katika kutoa taarifa muhimu kwa jamii zitakazopelekea kukua
kwa Sekta ya Elimu nchini. Pia amewataka wazazi kuwa mstari wa mbele na
kujitokeza kuhudhuria vikao katika shule na kutoa maoni yao kuhusu mambo
mbalimbali ikiwemo mitaala ya elimu na pia kushirikiana na redio za
jamii kwa kutoa taarifa muhimu na pia kuwahamasisha watoto wao na jamii
nzima kujenga utamaduni wa kusikiliza vipindi vya redio hizo kwa manufaa
yao.
Sehemu ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment