Thursday 22 August 2013

ABIRIA WALIOKUWA KWENYE NDEGE ILIYOANGUKA ZIWA MANYARA IKITOKEA BUKOBA WOTE WAMEOKOLEWA HIVI PUNDE

Habari zilizotufikia hivi punde mmoja wa wanasheria mahili nchini tanzania wakili Protas Ishengoma na wenzake ambao hatujajua idadi kamili waliokuwa kwenye ndege ya kukodi ya Tanzania air ikitokea bukoba leo asubuhi kuelekea dar na kuanguka ziwa manyara wameokolewa na wote wako katika hali nzuri,boti za tanapa na wadau mbalimbali wameshirikiana kuoko maisha ya abiria hao, wakili ishengoma walikuwa wakitokea kwenye msiba wa mama wa rafiki yao mpenzi joseph mushumbusi , ma herenestina aliezikwa jana kijiji cha kanazi bukoba.
bw kashasha mmoja wa abiria waliokuwa katika ndege hiyo, nae alikuwa akitokea msibani ,na yeye katika msiba huo ndio alikuwa mwendesha ratiba wa shughuli zote  za mazishi.

No comments:

Post a Comment