Friday, 5 July 2013

KESHO JUMAMOSI 6-07-2013 KAGASHEKI CUP KUANZA,KAGASHEKI KUYAFUNGUA RASMI AHAIDI ZAWADI NONO,BAKOBA KUFUNGUA NA HAMUGEMBE



Yale mashindano ya Kagasheki cup 2013 yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soko katika jimbo la bukoba manispaa yanatarajiwa kurindima kesho katika uwanja wa kaitaba kuanzia saa 9.00 alasiri.mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Marick Tibabimale amesema maandalizi yote yamekamilika na tayari kata zote 14 za jimbo la bukoba manispaa ziko tayari kwa mashindano. Akiongea kwa njia ya simu na redio kasibante mbunge wa jimbo la bukoba mjini ambae pia ni waziri wa maliasili na utalii balozi Khamis Kagasheki ambae ndio mfadhili wa kagasheki cup kwa asilimia mia moja amesema anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumpa afya njema na kuona anamjalia kuendelea kumpa nguvu ya kuendelea kufadhili mashindano haya kwa nguvu yake binafsi,amesema amekamilisha kwa kuzipatia timu zote jezi na mipira tena vifaa vya kisasa ili vijana waweze kucheza soka kwa uzuri,pia amewapatia jezi waamuzi wote watakoshiriki kuchezesha mechi,akiongelea upande wa zawadi amesema mshindi wa kwanza atapewa shilingi milioni tatu,mshindi wa pili milioni mbili na mshindi wa tatu milioni moja, lakini pia amesema zipo kata za ukanda wa kijani(green belt)kata nane mwaka huu atawapa pesa itakayowasaidia kwa ajili ya usafiri kila timu itapewa shilingi laki tano,ili waweze kuwahi michezo yote bila kuchelewa,lakini pia atalipia posho zote za marefa watakaochezesha,pia timu zote zitapata maji kwa ajili ya wachezaji, na misho akamalizia kwa kusema anawpenda sana wana bukoba na yeye atakuwepo katika ufunguzi. Mashinndano haya watu wote wataingia bure kwa maana gharama zote tayari mh kagasheki  kazitoa zikiwemo na za usafi wa uwanja.

No comments:

Post a Comment