Ni majira ya saa moja asubuhi bandari ya mwanza mv victoria imetia nanga ikitokea bukoba, watu wakishuka katika meli hiyo kuelekea maeneo tofauti,mara nyingi mnapokuwa melini si rahisi watu kuonana kwa pamoja kulingana na kila mmoja kuwa katika eneo lake lakini wakati wa kushuka ndo unaweza kumuona mwenzako na kutambua kuwa mlikuwa safari moja,meli hii ni kubwa inayobeba abiria pamoja na mizigo, hufanya safari zake kati ya mwanza na bukoba na bukoba na mwanza. mv victoria hutoka mwanza siku za JUMAPILI,JUMANNE NA ALHAMIS SAA TATU KAMILI na Bukoba ni siku za JUMATATU, JUMATANO NA IJUMAA SAA TATU KAMILI, hutoka bandari ya bukoba mjini kuelekea bandari ya kemondo na hapo uelekea mwanza
kushoto ni kaptan mwassa akifurahia baada ya kuifikishs salama meli ya mv victoria bandari ya mwanza akitokea bukoba
Ni abiria wakishuka kutokea bukoba,banbari ya mwanza
kushoto ni bahari shomari kitambo sana yumo melini
mrs magu
mdau maarufu kwa jina la magu akiwa na familia yake akitokea bukoba
meli ya mv victoria ni tegemezi kubwa kwa wakazi wa mwanza kupata ndizi, maharage,matunda kutoka bukoba
ndizi hizi na vitu vingine uenda mpaka mikoa ya shinyanga, mara,Tabota nk
ndizi za bukoba
abiria kila moja busy kuwahi anakoelekea
Usafiri wa meli mv victoria ni raha mustarehe
sasa tumifika tuwahi airport
yaani mteja alikuwemo , wewe vyumba vyote vilijaa...kilibaki kimoja nikalala mimi
leo watu walikuwa kibao...dah
tunashukuru tumefika salama ,shaiien vipi kwenu china kuna ziwa zuri kama hili...
wasafiri walipiga picha mbalimbali katika meli ya mv victoria
No comments:
Post a Comment