Wednesday 26 October 2016

BENKI YA POSTA TANZANIA(TPB) NA SBFIC WATEMBELEA MASHULE KARAGWE NA KUTOA ZAWADI.

 Katika maadhimisho ya wiki ya kuweka akiba duniani,Benki ya Posta Tanzania(TPB) na SBFIC pamoja na  washirika wake wametembelea shule mbalimbali za msingi na sekondari kujionea namna wanafunzi walivyoweza kufundishwa namna ya kujiwekea akiba benki kwa ajira ya matumizi ya badae,mbali ya kujionea namna wanafunzi hao walivyofundishwa, pia  SBFIC walitoa zawadi ya kalamu na daftari kwa wanafunzi waliojifunza,Shirika la Karudeca  kupitia Benki ya posta Tanzania wamekuwa wakitoa mafunzo katika shule hizo kwa kufadhiliwa na SBFIC.Shule zilizonufaika na mafunzo hayo ni Kayanga shule ya msingi, Ihanda sule ya msingi, Ndama shule ya sekonda, Kayanga shule ya sekondari na shule zingine wilayani Karagwe, Kilele cha maadhimisho ya wiki ya kuweka akiba kitafanyika siku ya Jumamosi 28-10-2016 katika uwanja wa mpira wa Kayanga kuanzia saa nne asubuhi,mbali ya viongozi mbalimbali  watakuwepo pia wasanii maarufu Mpoke wa Ze COMED na Bk Sande.(katika picha ni mtendaji mkuu wa SBFIC makao makuu Dar-es-salaam Bw  Marco Projosky akiuliza maswali  wanafunzi.)
 Katika ofisi za Karudeca maandalizi ya kutembelea mashule yakifanyika.

 Vitabu vya mafunzo vilivyotolewa na  SBFIC.
 Bi Karunde akimpa zawadi  ya shilingi elfu kumi mwanafunzi alijibu swali vizuri kuhusiana na namna ya kuweka akiba,
 Bw Miki Meneja wa Benki ya Posta Karagwe akitoa somo kwa wanafunzi.
  Zawadi zikitolewa.


No comments:

Post a Comment