*MATUKIO YA BARABARANI DAR ES SALAAM - ARUSHA
Fuso
lenye namba za usajili T 509 AGD, likiwa limeanguka na kumwaga mzigo
wote wa Nyanya uliokuwa umebebwa na fuso hilo. Haikuweza kufahamika kwa
haraka chanzo cha ajali hiyo.
Mmoja wa wahusika akijaribu kuomba msaada kwa magari yaliyokuwa yakipita eneo hilo.
Mafunzo
wa Kampuni ya Strabag, wakiendelea na kazi ya upanuzi wa barabara ya
Arusha inayoendelea kupanuliwa ambapo kwa sasa magari yamekuwa yakitumia
muda mrefu kumaliza eneo hilo kwa kupita katika barabara vumbi
iliyowekwa kwa dharula.
Upanuzi wenyewe ni kama hivi
Gari
ndogo inayoelezwa kuwa iligongwa na basi la Happy Nations eneo la Mto
Wami, likiwa limeegeshwa nje ya Kituo cha Polisi cha Wami.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mitaro katika barabara mpya ya mabasi ya Kaskazini, inayotokea Bagamoyo.
Jamaa wakilinda mzigo wao nyuma ua Canter, kutoka Soko la Kariakoo kuelekea Tegeta.
haikuweza
kufahamika jamaa hawa walikuwa wakisafiri kwa staili hii kuwa walikuwa
na matatizo ya kijamii au ndo tatizo la usafiri, hapa wakitokea bagamoyo
kuelekea Chalinze katika barabara mpya....
Ni
baadhi ya wachezaji wa Taswa Fc, waliposhuka kupata chakula cha mchana
maeneo ya Korogwe wakati wakielekea Mkoani Arusha kushiriki Bonanza
linaloandaliwa na Taswa Arusha kila mwaka.
Safari hiyo ilijumuisha timu zote mbili ya Taswa Fc na Taswa Queens....
Wachezaji wakishuka garini kuelekea kupata msosi....
Maeneo ya mbali na mijini hivi ndivyo vituo vya mafuta ambapo huuzwa kwa lita moja moja kama hivi...
Mafuta aina ya Petroli, yakiuzwa kwa staili hii jambo ambalo ni hatari....
*AJALI HAINA KINGA
Baadhi
ya abiria waliokuwa katika gari lililogongana na gari ndogo (pichani
chini) wakilia baada ya kutokea ajali karubu kabisa na maeneo ya njia
panda ya Kunduchi, wakati mabinti hao na wenzao wakiwa safarini kuelekea
Bagamoyo kama kundi kuhudhuria Bonanza la familia, mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Baadhi
ya abiria waliokuwa katika Coaster hilo, na mashuhuda wakijadili alaji
hiyo. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya magari kuumia.
*ANGALIA AKILI YA DEREVA HUYU v/s MNYAMA HUYU
Hapa
ilikuwa ni barabara mpya inayotokea Bagamoyo kuelekea mikoa ya
Kaskazini inayochomokea njia panda ya Chalinze, ambapo Mnyama huyu
alikuwa akikatiza barabara kuelekea upande wa pili wa barabara hiyo,
huku (kushoto) ni Lori lililokuwa katika mwendo na (kulia) mwa Lori hilo
ilikuwa ni Coaster iliyokuwa ikijaribu kulipita Lori hilo.
Wakati
Coaster ikikaribia kumaliza bodi ya Lori ndipo Mnyama huyu akatokea
upande wa pili akivuka huku akikimbia kwa mbwembwe akiruka ruka jambo
lililowafanya abiria waliokuwa katika Coaster kumfurahia huku
wakimsikitikia kuwa huenda asingewahi kuvuka kabla ya kulambwa tairi na
Lori.
Lakini
wakati abiria hao wakifurahishwa na Mnyama huyu ambaye alikuwa mithili
ya Nyani, ghafla Dereva wa Lori aliwashangaza watu baada ya kutumia bodi
kubwa ya Lori lake lililokuwa na tera 'Eti' kumkatia denge mnyama huyo
ili amkanyage na ndipo Lori hilo liliyumba na kutaka kuanguka huku
likitoka nje ya Barabara huku mnyama huyo akikatiza kiulaini na kuondoka
zake.
Sasa
sijui kama Dereva huyu angeangusha gari angejieleza alikuwa akifanya
nini, au angeelezeaje sababu za kuangusha gari. MADEREVA, UTULIVU, AKILI
NA BUSARA MUWAPO BARABARANI NDIYO KITU CHA KWANZA.
Hapa
Lori hilo likitoka nje ya Barabara kumkatia denege mnyama huyo, ambapo
lilimkosa na kuyumba wakati likijitahidi kurudi barabarani na kutaka
kusababisha ajali kwa kuigonga Coaster iliyokuwa pembeni yake.
*SALAAM ZA PONGEZI KUTOKA MMK MEDIA GROUP
Tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mwana habari mwenzetu ndugu Issa Michuzi na Blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com
kwa kazi kubwa walioifanya na wanayoendelea kuifanya ya kuhabarisha
jamii yetu kwa muda wa Miaka tisa (9) mfululizo bila kupumzika.
Blog ya Issa Michuzi imetimiza miaka 9 tangu kuanzishwa tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland. Kwanza
kabisa; tunampa hongera Ndugu Michuzi kwa kuandika historia kwa kuleta
mapinduzi ya habari ndani nchini na nje ya Tanzania.
Pili;
tumefurahishwa sana kwa kitendo cha Ndugu Michuzi kurudisha shukrani na
fadhila kwa Baba wa Ma-blog Bwana Ndesanjo Macha kwa kumtambulisha,
kumuingiza na kumfungulia blog ya jamii ya www.issamichuzi.blogspot.com
mnamo tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland.
Tatu;
Pongezi za kipekee zimuendee Ndugu Issa Michuzi kwa kazi kubwa ya
kutuhabarisha usiku na mchana pamoja na majukumu yake ya kikazi
akilitumikia vyema Taifa letu la Tanzania katika Ofisi Kuu kuliko zote
akiwa kama Mwanahabari Mpiga Picha (Photo Journalist) mwajiriwa wa
Serikali akifanya kazi chini ya Kurugenzi ya Mawasiliano, Ofisi ya Rais
Ikulu ya Tanzania.
Nne;
Ni ukweli usiopingika kwamba Issa Michuzi ni mtu wa watu, anapenda watu
na ucheshi wake umemletea mafanikio makubwa katika tasnia ya habari.
Kwa upande mwingine Michuzi ameitumia vyema nafasi ya kipekee aliyopata
kutuhabarisha kwa kutujuza mambo mbalimbali yanayoendelea ndani na nje
ya nchi. Hakuna ubishi tukijiuliza swali ni wafanyakazi wangapi waliopo
sasa hivi Serikalini katika nafasi kama ya Michuzi, ama waliopita ambao
wamefanya mapinduzi ya habari kama Michuzi?
Ndugu msomaji, ukweli unabaki palepale Michuzi anastahili pongezi za kipekee kwa kuthubutu.
Mwisho
kwa kumalizia napenda kuufahamisha Umma kwamba Bwana Issa Michuzi
amekuwa mfano wa kuigwa na jitihada zake na mazingira yake kikazi
yamekuwa chanzo cha mafanikio na umaarufu mkubwa aliojizolea na
kujijengea jina nchini na nje ya nchi. Hongera kwa jitihada na harakati
zako.
Tunatambua
pia kwa nafasi uliyonayo kikazi inakupa mlango wa kupata habari kabla
ya vyombo vingine vya habari kupata, na vilevile kwa kuwa mwajiriwa wa
Serikali umejijengea heshima kwa taasisi, wizara na vyombo vingine vya
Kiserikali kukuleletea habari zao moja kwa moja wewe kwanza kabla ya
vyombo vingine, kitu ambacho kimefanya watu wengi tuwe tunasoma blog
yako na kuipenda kitu ambacho ni kuzuri na cha kuigwa.
Mwisho tunakuomba ukaze mwendo na uendelee kutuhabarisha
No comments:
Post a Comment