Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Kufuata Kanuni za
Kiislamu (Islamic Banking), wa Benki ya NBC Tanzania, Yassir Masoud (katikati)
akizungumza katika droo ya awamu ya pili kupata washindi wawili waliojishindia safari
wao na wenza wao inayolipiwa kila kitu na NBC kushiriki ibada ya Hija mjini
Makka nchini Saudi Arabia baadae Mwezi ujao. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina
Maria Kimaryo, Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina na Mkaguzi Mwandamizi
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
Meneja Uhusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Eddie Mhina
akipiga simu kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya Islamic Banking ya benki hiyo
ambayo washindi wawili na wenzao wao watalipiwa gharama zote kwenda Makka
nchini Saudi Arabia kushiriki ibada ya Hijja baadae mwezi ujao. Wengine kutoka
kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo, Kaimu Mkuu wa
Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo
ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi
Abdulhussein (katikati) akihakiki majina ya washindi wa kampeni hiyo. Wengine
kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za
Kiislamu wa NBC, Yassir Masoud na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina
pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo.
Kaimu Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud (katikati)
akifurahi pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakati baadhi ya washindi
wakielezea furaha yao baada ya kupigiwa simu na kujulishwa kujishindia safari
ya kwenda hijja itakayolipiwa kila kitu na NBC. Kutoka kushoto ni Ofisa katika
Idara ya Operesheni, Edesia Kahyarara, Meneja Masoko, Alina Maria Kimaryo,
Meneja Uhusiano, Eddie Mhina na Mkaguzi
Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
No comments:
Post a Comment