Thursday 12 September 2013

CHUO CHA UALIMU-ERA KUANZA MAPEMA MWAKANI,NDOTO YA PASKAZIA BARONGO KUTIMIA

 Mkurugenzi wa kampuni ya passy community service Ltd Paskazia Barongo akiwakaribisha wadau wa elimu kutoka katika manispaa ya bukoba na maeneo mengine aliowakaribisha kuja kumpa mawazo,ushauri jinsi atakavyoanzisha chuo cha ualimu-ERA kinachotarajiwa kuanza mwakani mwezi wasaba katika manispaa  ya bukoba kata ya kitendaguro.Akiongea na wadau wa elimu bi paskazia barongo amesema anatarajia chuo wanachoanzisha kitakuwa cha mfano kwa kutoa elimu bora na kuigwa na vyuo vingine.
                                    baadhi ya wakuu wa shule za sekondari wakimsikiliza bi paskazia barongo
                                                               mdau amin akiwa na varelian
 mkurugenzi wa cosadakisikiliza kwa makini mipango ya uanzishwaji wa chuo cha ualimu mwakani
                          mzee kasimu,mmoja mwa wadau waliohudhulia mwaliko
 ni mchoro wa majengo ya chuo kitakavyokuwa kitakapokamilika,ila majengo yaliyopo wataanza nayo
                      bi paskazia barongo akiwatembeza wadau wa elimu kuangalia mazingira ya chuo
                 Bi paskazia barongo akieleza mikakati waliyonayo chuo kikianza mapema mwakani
                                                muonekano wa vyumba utakavyokua chuoni hapo
                                                              wadau ukiangalia maeneo ya chuo
                                                       majengo ya chuo ambayo yako tayari
                         chuo kitakuwa na eneo kubwa na mazingira ya kumuwezesha mwanachuo kusoma
                 picha ya pamoja ya wadau wa elimu walioudhuria mwaliko wa bi paskazia barongo
Ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu ya bi paskazia barongo anaeishi sweden kufanya kitu cha maendeleo nyumbani,sasa ndoto yake inaelekea kutimia mwakani kuanzisha chuo cha elimu,na kikubwa amesema si biashara lengo kuwapa elimu bora wanafunzi na kuelimisha jamii kwa ujumla. bi passy jamcobukoba.blogspot.com inakutakia afya njema,nguvu ili uweze kutimiza ndoto yako .

No comments:

Post a Comment