Tuesday, 1 April 2014
VURUGU ZILIZOTOKEA MECHI YA KAGERA SUGAR NA RUVU SHOOTING, KRFA WAMEJIPANGAJE KWENYE MECHI YA KAGERA SUGAR NA SIMBA JUMAMOSI 5-4-2014 KAITABA?
Kijana wa Kimasai alisababisha vurugu akiwa amezibitiwa na Polisi akiwa chini ya ulinzi
Wakati zikiwa zimesalia siku chache kufanyika mtanange mkali wa Kagera Sugar na Simba ligi kuu vadacom katika uwanja wa Kaitaba siku ya Jumamosi 5-4-2014 chama cha mpira Mkoa wa Kagera kimejipangaje kuhakikisha kinathibiti vurugu zinazoweza kutokea na kusababisha kuhatarisha usalama wa mashabiki,Katika mechi ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting iliyochezwa jumapili 30-3-2014 tumeshuhudia vurugu zilizozukiwa na Kijana mmoja wa kimasai aliemvamia shabiki mmoja alietambulika kwa jina la Moses Nyama ambae ni msanii katika bend ya muziki ya Kakau kumpiga akishilikiana na wenzake kwa fimbo huku wakiwa na siraha za visu viunoni na kumjerui kabla ya mashabiki kuingilia kati kumnusuru na badae Polisi kufika wakiwa wakitazama mpira badala ya usalama wa raia. Ili kuzibiti hali hii ya mashabiki kuingia uwanjani na fimbo, visu, mikuki nk KRFA na Jeshi la Polisi mmejipanga vipi katika mtanange wa Kagera Sugar na Simba Jumamosi 5-4-2014 ?
Huyu ni Mmasai ambae ni miongoni mwa waliojerui akiwa na sime kiunoni akizibitiwa na Askari waliovaa kilaia
Mashabiki wanahitaji Amani wakati wote uwanjani
Shabiki nguli wa Simba MSHAMU
Mmasai akiwa kapandisha mzuka anataka kupiga mtu na wengine wakiwa wamedhibitiwa na Mashabiki
Wote hawa wamasai walivamia mtu mmoja kwa fimbo zao ,na kumjerui
Mwenye kaunda suti ni Katibu wa KRFA Salumu Chama alilazimika kuingilia kati sakata hili
Baada ya dakika kadha Polisi waliokuwa wakiangalia mpira walikuja baada ya mashabiki kupiga kelele . Na hapa ndio swala la kujiuliza na kufanyiwa kazi, je Polisi anapoingia uwanjani ni kwa ajili ya kuangalia mpira au usalama wa mashabiki? swali kwa wahusika.
Je kuingia na fimbo na visu uwanjani ni sahihi?
Kulia ni Moses Nyama alipata kipigo kutoka kwa Wamasai Japo nae si haba MWANZONI alikabiliana nao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment