Wednesday 20 November 2013

JICHO LA CAMERA YETU BUKOBA MAENEO TOFAUTI LEO

 Ni maeneo ya Jamuhuri road karibu duka la vifaa vya ujenzi kwa Bandari dukani kwa Mh Murungi Kichwabuta akiwa na Mwl Bishanga(mwenye nguo nyekundu)wakiwa na mmliki wa  jamcobukoba.blogspot.com
 Enkonjwa au Gonja ni chakula kinachopendwa  na watu wengi sana, Aidha waweza kuzitengeneza kwa namna tofauti, waweza kuzichoma zikiwa mbivu, kuzikaanga au kuzichesha, au kuzichanganya na vyakula vingine.
                            Camera yetu maeneo ya soko kuu senene wameanza kupatikana
 Camera yetu maeneo ya kashai ,barabara iendayo kahororo  ni utaalamu wa kukamata senene,kama uonavyo ni teknologia ya kisasa inayotumika kukamata senene inayohitaji mtaji kwa kiasi fulani  kwa ajili ya kununua taa kubwa zenye mwanga mkali, mabati,mapipa au majaba makubwa, nishati ya umeme na rasilimali watu kwa ajili yakukusanya wanapokamatwa,kwa kipindi hiki watu wengi uingia katika biashara hii ambayo ukiifuatilia kwa karibu ni biashara ambayo inalipa na watu kujipatia kipato kikubwa ambacho kwa hali ya kawaida si rahisi kugundua kwa haraka.
 Camera yetu katika kanisa la mchungaji King James wa kashai ambae amejenga kanisa kubwa na la kisasa maeneo ya kahororo kyamaizi,Mchngaji King James amejizolea sifa rukuki kwa maubili yake na uponyaji kiroho na kwa muda mfupi kanisa lake kuwa na waumini wengi sana.
                           Mchungaji James (mwenye kofia) akiwa na Ramadhani kambuga
                                      waitu banyegere, jamani karibuni senene fresh wa leoleo
                                     kipindi hiki mabucha ya nyama hupata wakai mgumu
                                                          senene wakiwa wameshamenywa
                                              Kijana akiwajibika kumenya,akiwa katika ajira
                                                 Stand ya Tax soko kuu kwenye senene
 Vitu adimu maeneo mengine, lakini bukoba vinapatikana kwa wingi, entura,pilipili,namaharage mabichi
                Mh Murungi Kichwabuta akiwa amenunua pilipili mbuzi kwa matumizi ya nyumbani
 Wadada hao wawili wamejiajili kwa kutembeza ,pilipili.maharage,entura,entongo na vitu vingine kwenye maduka ya watu mbalimbali
                                                   Ongereni wadada kwa kujiajiri na kujitafutia kipato

No comments:

Post a Comment