Friday 22 November 2013

BALOZI KAGASHEKI ACHANGIA ZAIDI YA MILIONI NANE MRADI WA MAJI MTAA WA RWOME KATA YA KAHORORO LEO 22-11-2013

 Mbunge wa jimbo la bukoba mjini na waziri wa maliasili na utalii balozi Khamis Sued Kagasheki akiongea na wakazi wa mtaa wa rwome kata kahororo ambao wamekuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu. Baada ya mradi kuibuliwa na wanamtaa wa rwome  wenye thamani ya milioni 326 unaofadhiliwa na benki ya dunia,wananchi walitakiwa kuchangia asilimia 2.2 kiasi cha shilingi milioni tisa ili uweze kuanza,kitu ambacho kilishindwa kutekelezwa kutokana na hali ya ukata inayowakabili wananchi na kupelekea kupeleka ombi kwa mbunge wao ili aweze kuwasaidia.
 Mh mbunge  Kagasheki akiwasili kwenye viwanja vya zahanati kahororo akisalimiana na diwani wa kata hiyo Chief kalumuna
                                                                      Wanakahororo
                         Kulia wa kwanza Mwenyekiti wa ccm bukoba mjini Yusuf Ngaiza
                         Katibu wa chama bukoba mjini Bi Janat Musa akisalimia wanakahororo
                                                                wananchi wakifurahia
                               Diwani wa kahororo akiwa na mwenyekiti wa mtaa
           Wa pili kulia mzee muyoza aliewahi kuwa diwani wa kata ya kahororo kwa muda mrefu
 Bw bwemero akieleza mradi wa pikipiki unaodhaminiwa na Balozi kagasheki,amewataka vijana kufika ofisini kwao uswahilini mayunga ili waweze kupewa utaratibu wa kukopeshwa pikipiki
                                                           Watangazaji wa kasibante redio
                                                     Wanakahororo wakimsikiliza mbunge wao
 Balozi kagasheki pamoja na kuchangia mradi wa maji kwa wakazi wa rwome, pia amehaidi ndani ya wiki moja kuwanunulia tank kubwa la maji kwa ajili ya zahanati ya kahororo ,baada ya tank la zamani lililojengwa kuharibika,lakini pia kuna tatizo la ngedere wanaosumbua na kuharibu mazao ya wakazi wa kahororo na majirani, amehaidi kulipia gharama za milioni moja kuleta wataalamu waweze kukabiliana na tatizo hilo.
Mkuruganzi wa kiroyera Tours mama Mary Kalikawe nae alihaidi kuchangia dora 500 za kimarekani kuunga jitihada za balozi kagasheki kusaidia wananchi wa jimbo lake katika maendeleo

No comments:

Post a Comment