Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete akifunga bao la pili katika mchezo wao dhidi ya JKT Oljoro
HESABU zilizokuwa zikipigwa na wachezaji, viongozi,
benchi la ufundi na mashabiki wa Yanga, zimetimia na kufanikiwa kuongoza Ligi
Kuu Tanzania Bara katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.
Yanga walikuwa wakihitaji ushindi katika mchezo wao dhidi
ya Oljoro huku ikitaka mchezo kati ya Mbeya City na Azam uliochezwa Chamanzi
umalizuike kwa sare na hayo ndiyo yaliyotokea katika mchezo huo.
Mabao matatu yaliyofungwa na Simon Msuva dakika ya
23 na Mrisho Ngassa dakika ya 30 na lile la tatu lililofungwa na Jerry Tegete
yalitosha kuifanya Yanga imalize mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni baada ya
kutimiza pointi 28 baada ya kucheza michezo 13.
Katika mchezo wa Chamanzi Azam walilazimishwa sare
na Mbeya City ya mabao 3-3 na kuifungulia njia Yanga kukaa kileleni baada ya
kuwazidi kwa pointi mbili.
Azam na Mbeya City ambao walikuwa kileleni kwa
pointi 26 na sare hiyo timu zote sasa zimefikiwa pointi 27 huku Azam wakiwa
nafasi ya pili wakati Mbeya itakuwa nafasi ya tatu kwa tofauti na mabao ya
kufunga na kufungwa.
Nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo inashikiliwa na Simba wenye pointi 24 baada ya kushinda mchezo wake wa jana dhidi ya Ashanti United.
No comments:
Post a Comment