Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuzindua
rasmi Redio Jamii ya Wilaya ndogo ya Tumbatu visiwani Zanzibar. Kushoto
ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya
Umoja wa Mataifa (Unesco)Bw. Abdul Wahab Coulibaly wanaofadhili
unzishwaji wa redio za jamii Tanzania Bara na Visiwani.
Mkurugenzi
wa Kituo cha Redio Jamii cha Tumbatu Ali Khamis Mtwana akimpatia
maelezo juu ya utendaji wa Kituo hicho Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kukizindua rasmi.
Kulia
kwa Balozi Seif ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Unesco Bw. Abdul Wahab
Coulibaly na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali
Mbaouk.
Mkurugenzi
wa Kituo cha Redio Jamii cha Tumbatu Ali Khamis Mtwana akifanya vitu
vyake wakati akiwa hewani kurusha matangazo ya kituo cha Redio Jamii
Tumbatu mara baada ya kuzinduliwa na Balozi Seif Ali Iddi. Kushoto kwa
Balozi Sefu ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Elimu, Sayansi na
Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (Unesco)Bw. Abdul Wahab Coulibaly
wafadhili wa mradi huo.
Meza kuu
kutoka kushoto ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Elimu, Sayansi
na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (Unesco)Bw. Abdul Wahab Coulibaly,
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Sefu Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Unguja Pembe Juma Khamis, Waziri wa Habari Utamaduni Michezo
na Utalii Mheshimiwa Said Ali Mbarouk, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Issa Mlingoti pamoja na Afisa
Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi
ya UNESCO Yusuph Al-Amin.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na wananchi wa
Kisiwa cha Tumbatu katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Matangazo ya
Redio Jamii Kisiwani humo.
Na. Othman Khamis Ame
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Vituo vya Redio
Jamii hapa Nchini vinapaswa kuwa chem Chem ya elimu itakayotoa manufaa
kwa Jamii inayovizunguuka Vituo hivyo badala ya utaratibu wa kurusha
vipindi vya muziki wakati wote.
Kauli
hiyo aliitoa wakati akiizindua Redio Jamii ya Wilaya ndogo ya Tumbatu
hapo katika jengo la Wilaya hiyo liliopo katika Kijiji cha Kichangani
ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 50
ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Balozi
Seif alisema mijadala na nakala zinazohusiana na masuala ya Uchumi,
siasa, jamii na Maendeleo ndio lengo lililokusudiwa katika uanzishwaji
wa Redio hizo na kupelekea kuungwa mkono na Taasisi na mashirika ya
maendeleo Duniani.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka watendaji wa Redio Jamii Tumbatu
kujitahidi kuwaelimisha wananchi kuhusu uvuvi bora na mambo mengi
yanayohusiana na bahari kwani maisha ya wananchi hao yametegemea zaidi
sekta ya bahari.
Wakazi
wa Tumbatu wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Pili Balozi Sefu Ali Iddi
wakati akisoma hotuba yake kwenye sherehe ya uzinduzi wa Redio Jamii ya
Tumbatu.
Kaimu
Mwakilishi Mkazi Mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano
ya Umoja wa Mataifa (Unesco)Bw. Abdul Wahab Coulibaly akitoa salamu zake
katika hafla ya ufunguzi wa kituo cha redio jamii Tumbatu kilichopata
msaada na ufadhili mkubwa kutoka shirika hilo.
Bw. Coulibaly amesema Redio waliyoikabidhi ni ya tatu kwa Zanzibar baada ya zile za Micheweni na Makunduchi huko kusini Unguja.
“
Tunategemea redio yenu ya jamii hapa Tumbatu itajikita zaidi katika
kuwaelimisha wananchi wa Kisiwa hichi na maeneo ya jirani kuhusu athari
za uvuvi haramu ambao unapigwa vita na Serikali kisheria “. Alisisitiza
Balozi Seif.
Alitahadharisha
jamii kwamba vyombo vya habari vina nguvu kubwa ambayo kama itatumika
vibaya inaweza kuleta mifarakano mikubwa katika jamii na hivyo basi
usalama na amani unaweza kuhatarishwa.
Balozi
Seif alifahamisha kuwa chokochoko na fitna za kisiasa zikiachiwa na
kuelekezwa katika vituo vya redio Jamii ni mwanzo wa kuathirika kwa
vituo hivyo, watendaji pamoja na wananchi wenyewe.
“ Nia ya
Redio jamii ni kuelimisha jamii na sio kupotosha. Hivyo Wanahabari wa
Redio hizi wanapaswa kufanya utafiti wa kina wa Habari zao kabla ya
kuzitoa, vyenginevyo zinaweza kupotosha jamii “. Alifafanua Balozi Seif.
Alileza
kwamba lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona vyombo vya
Habari na utangazaji nchini vinasaidia kudumisha na kuimarisha usalama
na amani hatimae kupata maendeleo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka watendaji wa Redio hiyo redio
nafasi kwa wananchi wa rika, jinsia na kila makundi yote yanayostahiki
kusikika katika jamii inayowazunguuka.
Waziri
wa Habari Utamaduni Michezo na Utalii Mheshimiwa Said Ali Mbarouk
akisoma risala yake kwa wakazi wa Tumbatu kwenye sherehe za ufunguzi wa
redio jamii kisiwani humo.
Balozi
Seif alilishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa
Mataifa {UNESCO } kwa msaada wake mkubwa wa vifaa vya studio na mitambo
ya kurushia matangazo kwa Redio Jamii ya Tumbatu.
Aliiomba
taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa kuendelea kusaidia harakati nyengine
za kijamii kila hali inaporuhusu na kitendo cha Uongozi wa Jumuiya hiyo
kuahidi kukamilisha changamoto zinazokikabili kituo hicho ndani ya mwezi
mmoja ujao ni cha kupigiwa mfano.
Akisoma
Risala ya Wananchi wa Kisiwa hicho Afisa Tawala wa Wilaya Ndogo ya
Tumbatu ambae pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Redio hiyo Ndg. Mohd Omar
Hamad alisema uongozi wa Redio hiyo umekusudia kutoa vipindi
vitakavyotumiwa na wanafunzi wa Maskuli na Madrasa za eneo hilo.
Afisa
Tawala wa Wilaya Ndogo ya Tumbatu ambae pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Redio hiyo Ndg. Mohd Omar Hamad akisoma taarifa yake mbele ya mgeni
rasmi.
Ndg.
Mohd alisema utaratibu huo ambao ni miongoni mwa mpango kazi wa Redio
hiyo utasaidia wanafunzi hao kujiimarisha zaidi kielimu kwa kujijengea
uwezo mkubwa wakati wanapokabiliana na mitihani yao.
Hata
hivyo Afisa Tawala huyo wa Wilaya ndogo ya Tumbatu alielezea changamoto
zinazokikabili kituo hicho cha Redio jamii Tumbatu ikiwa ni pamoja na
ukosefu wa jengo la kudumu ambapo hivi sasa wanatumia jengo la Ofisi
ya Wilaya hiyo.
Akitoa
Salamu za Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa {
UNESCO } Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo Bw. Abdul Wahab
Coulibaly alisema Taasisi yake itaendelea kushirikiana na washirika
wengine wa maendeleo katika kuunga mkono Vituo vya Redio Jamii.
Bw.
Abdul Wahab Coulibaly alisema Redio Jamii Tumbatu iliyopata ufadhili wa
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la Unesco ina uwezo wa nguvu za Walti
300 ambazo zinaweza kuhudumia wasikilishaji zaidi ya Laki 150,000.
Akimkaribisha
mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk alisema Redio
Jamii Nchini tayari zimeshaonyesha mafanikio makubwa kwa kuisaidia
kubadilisha mazingira ya Jamii kupitia taaluma inayotolewa kwenye
vipindi vya Vituo hivyo.
Waziri
Mbarouk alifahamisha kwamba Zanzibar hivi sasa ina vituo ishirini vya
matangazo ya redio ikilinganishwa na kituo kimoja tuu cha Redio cha
Serikali { STZ } kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Wanatumbatu wakitoa burudani ya Kaswida wakati wa sherehe za uzinduzi wa redio ya Jamii Tumbatu.
Alieleza
kwamba kadri hali ya maisha inavyobadilika ndivyo sekta ya Habari
inavyopanuka ikitoa fursa pia kwa redio nyengine za Jamii zilizoanzishwa
katika Wilaya ya Micheweni Pemba na Mtengani Makunduchi Kusini Unguja
kwa msaada mkubwa wa UNESCO kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
Redio
Jamii ya Kisiwa cha Tumbatu inayotumia masafa ya 94.99 F.M inasikika
katika umbali wa Kilomita zaidi ya 15 unaokizunguuka kituo hicho. Hata
hivyo Redio hiyo pia inawqeza kusikika hata katika eneo la Mji wa
Zanzibar kutegemea hali ya hewa iliyopo.
Wakazi wa Tumbatu wakicheza Kaswida kwa furaha bila kujali Mvua kali iliyokuwa inanyesha kisiwani hapo.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na Utalii visiwani
Zanzibar Mh. Hindi Hamadi akiwatunza mabinti waliokua wakitoa burudani
ya kughani mashairi wakati wa sherehe hizo.
Sehemu ya wakazi wa wilaya ndogo ya Tumbatu kwenye sherehe hizo.
Afisa
Tawala wa Wilaya Ndogo ya Tumbatu ambae pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Redio hiyo Ndg. Mohd Omar Hamad (mwenye suti ya kijivu) akiutambulisha
Uongozi na wafanyakazi wa Redio Jamii ya Tumbatu kwa mgeni rasmi makamu
wa Rais wa Pili Zanzibar Balozi Sefu Ali Iddi (hayupo pichani)
Makamu
wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Kaimu Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (Unesco)
Bw. Abdul Wahab Coulibaly wakiondoka eneo la tukio mara baada ya
kuzindua rasmi redio jamii ya Tumbatu.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Issa
Mlingoti(kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango Taifa wa
Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph
Al-Amin mara baada kumalizika kwa sherehe za uzinduzi wa redio jamii
wilaya ndogo ya Tumbatu visiwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment