Sunday 3 November 2013

MASHINDANO YA MBIO ZA MITUMBWI YA BALIMI MKOA KAGERA YAFANA


Mashindano ya mbio za Mitumbwi mkoa wa Kagera  ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager zimefanyika leo katika fukwe za Spice Hotel mjini Bukoba, washindi kupatikana na kukabidhiwa vitita vya zawadi. Ambapo Fainali ya kanda yatafanyika Jijini Mwanza mwezi ujao tarehe 7 december, 2013.
Huduma ya kutoa vifaa kwa ajili ya kujikinga ikiendelea kabla ya mashindano kuanza
Vijana kazi wakianza kujiandaa kabla ya mtanange huo mkali wa kusaka washindi wa kuwakilisha kwenye  huko jijini Mwanza tarehe 7/12/2013
Mitumbwi ikishakaguliwa na hapa ni kuingia tu kuanza mashindano rasmi
Katika kuchukua matukio ya bukobasports.com ilibidi na mimi nivae kama mwanamshindano ili niweze kuchukua picha vizuri tayari kufukuzana na mashindano hayo makubwa ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager.
Kazi imeanza...
Ilichukua muda wa dakika kama 40 kwenda mpaka mwisho na kugeuza kurudi walipoanzia
Mgeni rasmi RPC Kagera(katikati) ACP-Philip Kalangi (katikati), kulia ni Mwenyekiti Makasia mkoa wa Kagera Bw. Faraji Mugaye na (kushoto) ni Mwenyekiti Makasia Taifa Bw. Richard Mgabo
Mashindano yakiendelea pia kulikuwa na burudani safi zikiendelea hawa ni Vijana wa hapa Bukoba wanajulikana kwa jina la wasafi..
Kila mtumbwi ulitaka ushinde na kunyakua kitita


Burudani ikiendelea..




Wanawake nao walikuwepo kwenye mtanange huo mkali wao raundi yao walikuuwa na mitumbwi 12
Sehemu ya mwishoni lazima upite nje ya bendela hiyo nyeupe na kutafuta nyingine na kugeuka ulipotoka!
Wanawake wakiwajibika kutaka kupata ushindi hapa




Wanawake hao wakipiga Kasia kwa kwenda mbele!!

Wazungu nao walikuwepo kushuhudia mitanange hiyo

Ilikuwa ni patashika!!.

Jamal Kalumuna kulia akiwa na kiongozi
Mdau wa Michezo na Mwana Bukoba Veteran Bw. Ernest Nyambo nae alikuwepo
Wadau

Picha ya pamoja ya Wadau.
Sehemu ya meza kuu.Bingwa mtetezi ni Kagera, Kombe la mwaka 2012 na sasa lilikabidhiwa kwa Mgeni rasmi
Washindi wa Mwaka jana nao walikuwepo kushiriki mashindano hayo na bingwa mtetezi alitoka mkoa huu wa Kagera wa mwaka jana 2012 hivyo mashindano hayo yatakayo fanyika mwanza mwezi ujao tarehe 7 december nao watashiriki mashindano hayo. Ambapo washindi wanne wamepatikana.
Wakikabidhi kombe la mwaka jana 2012 kwa Mgeni Rasmi RPC Kagera(katikati) ACP-Philip Kalangi
Wakati wa Zawadi
Wanawake walioshinda ni wale waliokuwa wanaongozwa na Levina Constantine na Salome Ernest.
Ushindi mtamu: Mshindi wa kwanza kwa wanawake alipewa kitita cha Tsh: 700,000/=  hapa ilibidi wacheze ngoma ya Saida Maana walifurahi sana.
Picha ya pamoja ya washindi Wanawake  na viongozi ambapo walioshinda ni mtumbwi uliokuwa na mkuu wao Bi. Levina Costantine kutoka Bushasha Bukoba Vijijini. Mshindi wa pili ni Bi. Salome Ernest kutoka Musila
Washindi wakionesha vitita vyao
Ushindi raha jamaniiii..
Picha ya pamoja washindi Wanaume na Viongozi, Wanaume walioshinda ni Delius Kiiza, Eliud Prosper, Zaidock Kaiza, Emmanuel Petro, Dastan Petro, Eliakim Zaidock, Nashow Bakuza, Frolence Kiiza, Edwin John na Johansen Paulo wa Izigo Muleba.
Picha ya pamoja ya Viongozi.

Zawadi zilikuwa hivi:-
Mshindi wa kwanza kwa      Wanaume                   Wanawake
                                         1-  900,000/=                700,000/=
                                         2-  700,000/=                 600,000/=
                                         3-  500,000/=                 400,000/=
                                         4-  400,000/=                 300,000/=

No comments:

Post a Comment