Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa kwenye mazungumzo ya
awali na Mkuu wa Shule ya Arusha (Madam Kitigwa) baada ya kuwasili
katika shule hiyo kwa lengo la kukutana na Kilabu cha Umoja wa Mataifa
shuleni hapo na kuzungumza na Wanafunzi kuhusiana na agenda mbalimbali
za Umoja huo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na
Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya
kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la
kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
Afisa
Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na wanafunzi-wananchama wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika
Shule ya Msingi Arusha Medium ambapo amewasisitiza juu ya umuhimu wa
kuzifahamu agenda mbalimbali za Umoja Mataifa na nafasi yao katika
kuleta maendeleo chanya kwa jamii.
Mwenyekiti
Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN)
Bw. Rahim Rajab Nasser akizungumza na vijana wa shule ya msingi Arusha
Medium juu ya umuhimu wa vilabu hivyo na umuhimu wa ushiriki wao kuanzia
shule za msingi mpaka Sekondari na Vyuoni.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
(katikati) akisisitiza jambo kwa vijana wa shule ya msingi Arusha
Medium. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba ya kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha na kushoto Mwenyekiti Taifa wa Vilabu
vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab
Nasser.
Kobe
mwenye umri sawa na shule ya Msingi Arusha Medium iliyojengwa mwaka
1930 akiwa hai mpaka na kuwa kivutio kwa wageni mbalimbali wanaofika
shuleni hapo ikiwemo Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa
(YUNA/UNCTN).
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha kuhusiana na umuhimu
wa agenda za malengo ya Milenia (MDG's) yanayotarajia kufikia tamati
2015 ambapo wao kama vijana wameshauriwa kutilia mkazo utekelezaji wa
malengo hayo ikiwemo Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa Wanawake,
Upatikanaji wa Huduma bora za uzazi na kupambana na Ukimwi, Malaria na
magonjwa mengine.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha
waliobahatika kushiriki mkutano huo ulioendeshwa na Wajumbe wa kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa
Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
akisalimiana na Mkuu wa Shule ya USA Academy Bw. Elibariki Malisa mara
baada ya kuwasili shuleni hapo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika
ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa
lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa na mwenyeji wa
msafara wao MC Kalinga wa Arusha wakielekea kukutana na wanafunzi wa USA
Academy.
No comments:
Post a Comment