Thursday 24 October 2013

CHAMA CHA WAPISHI CHAANDAA TAMASHA KWA WATOTO YATIMA


Baadhi ya wapishi katika hotel maarufu jijini Arusha wakiwa wanajadiliana wakati Tamasha la watoto yatima na walemavu wa viungo likiwa linaendelea ambapo siku hiyo ilikuwa imeandaliwa na chama cha wapishi duniani lengo ni kuwaleta pamoja watoto.

Watoto waliofika katika tamasha hilo ambapo zaidi ya watoto 300 walishiriki kutoka sehemu mbalimbali jijini Arusha

Mtoto Daudi Izrael Mshana mwenye ulemavu wa utindio wa ubongo(12)akiwa amepakatwa na mama yake Belinda Izrael katika tamasha la watoto katika hotel ya Mt.Meru jijini Arusha

Watoto wakiwa wanaimba nyimbo ya huzuni iliyokuwa imebeba ujumbe kuhusu watoto yatima

.Mustapha na Ibraa Mhinda ni watoto waliokuja kujumuika pamoja na watoto yatima ambapo kwa nyakati tofauti walitoa rai kwa jamii kuwathamini watoto wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwapa mapenzi mema,malazi,mavazi,elimu na chakula bora

.Chef Tom akiwa anaongelea juu ya tamasha hilo na vyombo vya habari ambapo alisema kuwa jamii imesahau kwa kiasi kikubwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na walemavu

Kushoto Mkurugenzi wa Bearfoot entainment Dorothy Mustapha akiwa anawakabidhi msaada wasimamizi wa vituo vya watoto yatima

Picha ikimuonyesha msemaji wa World Chef day Chef Method Mrosso akiwa anawakatia keki watoto wanaoishi katika mazingira magumu,mwishoni mwa wiki jijini Arusha katika hotel ya Mt.Meru siku ambayo chama cha wapishi duniani hujutolea kwa kuwapikia na kula pamoja

.Baadhi ya wapishi wakiwa katika picha ya pamoja .(Picha zote na Pamela Mollel wa jamiiblog.co.tz)

No comments:

Post a Comment