Beki
wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel
Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa Dar es
Salaam.
Katika
mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3, ambapo Yanga ilipata
mabao yake katika kipindi cha kwanza kupitia kwa wachezaji Mrisho Ngasa,
aliyetupia katika dakika ya 15, Hamis Kiiza 36 na 45.
Mabao
ya Simba yalifungwa kipindi cha pili kupitia wachezaji wake, Betram
Mwombeki, katika dakika ya 54, Joseph Owino katika dakika ya 57 na
Gilbert Kaze, katika dakika ya 83.
Baada
ya Simba kusawazisha mabao yote matatu viongozi na mashabiki wa timu
hiyo walionekana kushangilia sare hiyo, ambayo kila mmoja aliyekuwapo
uwanjani hapo hakuweza kuamini kilichotokea kuanzia mashabiki, wachezaji
wa Yanga na hata wa Simba.
Mashabiki wa Simba, walikuwa kama wamemwagiwa maji, wakiwa na huzuni katika kipindi cha kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0.
Mshambuliaji Mrisho Ngasa, (kulia) akimtoka beki wa Simba, Joseph Owino, katika kipindi cha pili.
Mshambuliaji
wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba, Joseph
Owino na Gilbert Kaze, katika kipindi cha kwanza.
Mrisho Ngasa, akiruka kwanja la beki, Gilbert Kaze.
Mashabiki wa Yanga ilikuwa ni furaha kama hivi, ambapo baadaye furaha hii ilizimika ghafla.
Katika
mtanange huo, mashabiki kadhaa walizimia, ambapo shabiki huyu wa Yanga,
akibebwa kutoka jukwaani baada ya kuzimia, huku mashabiki saba wa Simba
na wawili wa Yanga walizimia.
Mshabiki wa Simba walizinduka na kushangweka kama hivi, baada ya kupata bao la pili.
Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake la kwanza alilofunga katika dakika ya 15, kipindi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment