Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Wilfred Muganyizi Rwakatare kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaoishi Bukoba na wanaoishi nje ya Bukoba wameandaa Kongamano kubwa lakujadili dhima ya Maendeleo ya mji wa Bukoba litakolofanyika 27-12-2015 kuanzia saa 9.00 Alasili katika ukumbi wa St Thereza Bukobawakatare, Kongamano linatambulika kama BUKOBA MUNICIPAL,DEVELOPMENTAL,CONFERENCE(BUMUDECO)Mh Rwakatare ambae ndie mratibu wa Kongamano hilo amesema shughuli zitakazofanyika na malengo yanayokusudiwa kufikiwa katika Kongamano hilo ni pamoja na kuwasilisha mpango kazi wa Mbunge na Baraza la madiwani la Manispaa ya Bukoba kwa kipindi cha mwaka 2015-2020 kama walivyoahidi wakati wa kampeni, Kubainisha fursa za biashara,uchumi na maendeleo zinazopatikana ndani ya Manispaa ya Bukoba,kupokea mada na michango kutoka kwa wanataaluma,wawekezaji na wajasiriamali mbalimbali na washiriki wa Kongamano kwa ajili ya kupeana ufahamu na uzoefu,Mh Rwakatare ameendelea kusema kuwa Kongamano hili litakuwa na watu kutoka nje ya nchi wanaBukoba na wasio wanabukoba wadau wa maendeleo,amewaomba watu wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuweka mipango ya kuipeleka mbele Bukoba kwa maendeleo ya haraka,bila kujari itikadi za kisiasa Bukoba kwanza.(katika picha mmiliki wa mtandao wa jamcobukoba.blogspot.com mwenye koti la draft akifanya mahojiano na Mh Mbuge wa jimbo la Bukoba mjini Wilfred Rwakatare)
Katika mahojiano
usikose 27-12-2015 katika Kongamano la maendeleo ya Bukoba.
No comments:
Post a Comment