Saturday 2 July 2016

WANAPAMOJA GROUP WAMUAHANI MWENZAO DOTO RAMADHANI (MAMA RUBI) KWA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

 Wanachama wa umoja wa kusaidiana katika raha na shieda Pamoja group wamekwenda kumuahani mwanaumoja mwenzao Doto Ramadhani maarufu Mama Rubi aliempoteza mama yake mzazi(aliefariki) wiki moja iliyopita na kuzikwa huko mkoani Tabora,Wanapamoja group walifika nyumbani kwa mama Rubi Hamugembe Kashabo  Bukoba  na kushiriki futari kwa pamoja na baada ya hapo kukubidhi rambirambi zao.(katika picha mwenyekiti wa pamoja group wa kwanza kulia akiwa na katibu Prisilla Mwainunu wakikabidhi kiasi cha zaidi  ya shilingi milioni mbili kwa mfiwa mama Rubi mwenye ushungi wa njano) umoja huu una wanachama wasiozidi 40.
 Wanapamoja wakiwasili nyumbani kwa mama Rubi kashabo Bukoba mjini.


Daima pamoja group katika ubora wao.

No comments:

Post a Comment