Saturday, 2 July 2016

MTANZANIA ALIYEIBUKA MSHINDI WA KWANZA AFRIKA NA WA SITA DUNIANI KATIKA MASHINDANO YA KUSOMA QUR-AN KWA NJIA YA TAJIWEED AWASILISHA TUNZO KWA MZEE MWINYI



Mwanazuoni kutoka Kondoa, Tanzania, Sheikh Rajay Ayub ambaye ameibuka mshindi wa kwanza Afrika na wa sita Duniani katika mashindano ya 37 ya Kimataifa ya usomaji Qur-an kwa njia ya Taj-weed, yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Iran akikabidhi tuzo zake kwa Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla ya kumpongeza iliyofanyika leo, kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania-BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam. Kulia ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakary Bin Zubeir na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa, Alhaj Omary Kariati ambaye aliratibu hafla hiyo. 

No comments:

Post a Comment