Friday, 4 October 2013

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH. KAGASHEKI AONGOZA MATEMBEZI YA SIKU YA TEMBO DUNIANI JIJINI ARUSHA YALIYO CHUKUA ZAIDI YA KILOMETA 4 LEO.


 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya Tembo hao.
 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akionesha moja ya vibao ambavyo vinawaonesha Tembo wakati wa Matembezi hayo ya amani.
 Kutoka kushoto ni Mrs. Tibaijuka akifuatiwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki,Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Willbert Chambulo, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo.
 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa katika Matembezi ya Siku ya Tembo Duniani
 Baadhi ya Wanaharakati wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani
 Ma elfu ya Wananchi kutoka Arusha pamoja na wadau wengine kutoka Mikoa na nchi mbalimbali wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani yaliyo Fanyika Arusha Leo
 Hawa ni Watoto Shupavu kabisa waliojitolea Mstari wa mbele katika Matembezi ya Tembo leo
 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akisaini katika moja la bango la siku ya Tembo , ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu
 Maandamano yakiwa yanaendelea
 Wa kwanza kutoka kushoto ni Mr. Peter ambaye ndiye alikuwa katika kamati kuu ya Maandalizi ya Siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, na pia Makamu mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours operators akiwa katika matembezi hayo
 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akiongoza Ma elfu ya watu wakiingia katika viwanja vya AICC ambapo ndipo ilikuwa kilele cha Matembezi hayo
 Afisa Mtendaji wa Chama cha Wakala wa Utalii TATO Ndugu Sirili Akko akitoa Maneno machache kabla ya ufunguzi Rasmi wa Kilele cha Matembezi ya Tembo Duniani.
 Meza kuu wakiongozwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki wa nne kutoka kushoto wakiwa wamesimama kwa mda wa dakika moja kuwakumbuka Waliokufa katika Tukio la Westgate Kenya pamoja na Tembo walio uwawa .
 Mc akiwa anaanza Tukio rasmi kwa kuwakaribisha viongozi mbalimbali kwa ajili ya Kutoa salam zao na Risala
 Dr. Alfred kikoti Akitoa Mada yake juu ya Idadi ya Tembo ambao wamebakia , pia kuelezea kutokomeza kwa Biashara haramu ya uuzaji wa uuzaji wa Meno ya Tembo, na kusisitiza Tanzania inategemea Tembo katika Utalii.
Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Ndugu Wilbert Chambulo akielezea juu ya kusimamisha biashara kubwa ya Meno ya tembo ambayo inaongozwa na Nchi ya China na kuziomba Nchi zengine kusimamisha Biashara hiyo Haramu .
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya  Mongela wa Arusha Akimkaribisha Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo akiwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushiriki kikamilifu zoezi la matembezi ya siku ya Tembo Duniani na kumkaribisha Mgeni Rasmi Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki  kutoa hotuba yake.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akizungumza na wanaharakati waliofika katika siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, kwa kutoa Salamu kutoka kwa Muheshimiwa Rais Kikwete kwamba Oparesheni ta kutokomeza majangili imeanza na Haitasimama, alisisitiza kwamba Wanasheria wafunge midomo yao kuhusu kutetea haki za binadamu , Aliongeza kwamba majangili wauwawe huko huko wakikamatwa kurahisisha msongamano wa kesi mahakamani, na Mwisho aliongeza kwamba Wanasiasa wasiingilie swala hili la kupambana na ujangili.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akikabidhi vyeti kwa Shule Zilizo Shiriki Katika Matembezi ya Tembo Duniani
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akipokea zawadi kutoka kwa TATO Anaye mkabidhi zawadi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa TATO Mr. Peter
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mlongo akipokea zawadi kutoka TATO Anayemkabidhi ni Bi. Tibaijuka
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa Ndugu. Allan Kijazi akitoa neno la Shukurani wakati wa kufunga Kilele cha siku ya Matembezi ya Tembo Duniani leo
Hawa ni Wale waliotembea katika Matembezi ya Kupinga mauaji ya Tembo Kutoka Arusha hadi Dar es salaam Mwendo wa Kilometa 650 kwa Siku 12 Kutoka kushoto ni Binti Mdogo mwenye umri wa Miaka 20 Kaptorina Manange,Mkazeni Y. Mkazeni, Rehema Y. Najema, na Livingstone Y. Mkazeni.

Maandamano haya yalitokea Jirani na Cultural Heritage Hadi Viwanja vya AICC Kijenge Jijini Arusha, Matembezi yaliyo andaliwa na Tanzania Association Tours Operators (TATO)

No comments:

Post a Comment