Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na
Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji
na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kolobelo unashiriki Mkutano wa 36 wa
Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa
Afrika (SADC), nchini Swaziland.
Mkutano
huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Swaziland, Dkt. Sibusiso Dlamin
umehudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Malawi, Zambia,
Zimbabwe, Lesotho, Swaziland, Botswana, Msumbiji, Namibia, Seychelles,
Botswana, Madagascar na Mauritius.
Mkutano huo umeanza tarehe 8 Julai, 2017 na utamalizika tarehe 11 Julai, 2017.
Waziri
Mkuu wa Swaziland, Dkt. Sibusiso Dlamin akifungua Mkutano wa 36 wa
Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC) unaofanyika nchini Swaziland.
Ujumbe
wa Tanzania unaoshiriki mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Swaziland,
kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji,
No comments:
Post a Comment