WANANCHI WAIOMBA SERIKALI IONGEZE MUDA ZAIDI WA KULIPA KODI YA MAJENGO
Zikiwa
zimebaki siku tatu kati ya siku 15 zilizoongezwa na Serikali kwa
wananchi kulipa kodi ya majengo bila adhabu, baadhi ya wakazi wa Jiji la
Dar es Salaam wameiomba Serikali iongeze muda mwingine zaidi ili watu
wote waweze kulipa kodi hiyo bila adhabu kutokana na changamoto
mbalimbali zilizojitokeza wakati wa zoezi hilo.
Wananchi
hao wamemweleza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
alipofanya ziara za kushitukiza katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA-Mtaa wa Kipata-eneo la Mnazi Mmoja na Mbagala mkoani Dar es
Salaam
Wamesema
kuwa mwamko wa wananchi kulipa kodi ni mkubwa hali iliyosababisha
foleni kubwa kila mahali nchini kutokana na uhaba wa watumishi wa TRA
pamoja na vitendeakazi muhimu kama vile kompyuta na mashine za
kielektroniki za kutolea risiti (EFDs).
Waziri
wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango amewataka Watanzania kuwa
watulivu na kuendelea kulipa kodi hiyo huku akiahidi kutatua changamoto
ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendeakazi ili kuwaondolea adha
wananchi waliojitokeza kwa moyo kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ya
majengo.
Ameahidi
pia kwamba Serikali itayafanyiakazi maombi ya wananchi ya kutaka
kuongezewa muda wa kulipa kodi hiyo na kwamba watajulishwa wakati
muafaka uamuzi wa Serikali kuhusu suala hilo.
Dokta
Philip Mpango amesema kuwa Serikali inafarijika kwa kiasi kikubwa na
namna wananchi walivyoitikia wito wa Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe
Joseph Magufuli unao wataka wananchi walipe kodi kwa ajili ya maendeleo
ya Taifa.
Amebainisha
kuwa watu wanapolipa kodi wanaipa nguvu Serikali ya kuboresha huduma za
jamii kwa wananchi ikiwemo elimu, barabara, maji, afya na kuboresha
huduma ya umeme hususan vijijini na kulifanya Taifa kupunguza utegemezi
wa misaada kutoka nje ya nchi.
Majuma
mawili yaliyopita Serikali iliongeza muda kwa wananchi kulipa kodi ya
majengo bila adhabu kwa muda wa majuma mawili hadi Julai 15 mwaka huu
ambapo siku hizo zitaisha siku ya Jumamosi huku idadi kubwa ya watu
ikiwa bado wanahitaji kulipa kodi hiyo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto)
akiongea na wananchi waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi
za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)-Ilala Mtaa wa Kipata, na kuwapongeza
kwa kuitikia wito huo kwa wingi na kuwaeleza kuwa kwa kulipa kodi
kutasaidia upatikanaji wa huduma muhimu kama maji, barabara, umeme na
dawa hospitalini.
Wananchi
waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa
wa Kipata, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb), (kulia) akiwaelezea namna atakavyoboresha huduma kwa
walipa kodi za majengo kwa kuwapa kipaumbele walemavu, wazee, wagonjwa
na wasiojiweza. Tukio hili litaenda sambamba na kuwawekea sehemu maalumu
ya kukaa wakati wakisubiri huduma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto)
akipokea shukrani na pongezi kutoka kwa Bi. Rose Muyalo, kwa utendaji
makini wa Serikali ya Awamu ya Tano na kwa kupatiwa huduma bora kutoka
kwa wafanyakazi wa TRA.
Bw.
Obedi Hezron Misoji (kulia) ambaye ni mstaafu akimuomba Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), kuongeza muda
wa zoezi hili la ulipaji kodi ya majengo kwani watu bado ni wengi na
Watanzania wameonesha nia yakujitokeza kwa wingi kulipia kodi hiyo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia)
akiongea na wananchi waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata kulipa kodi za majengo na kuelezea
furaha yake namna walivyoitikia wito huo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto),
akiwasikiliza viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa
Kipata namna ambavyo wanaweza kukabiliana na changamoto wanazokabiliana
nazo katika zoezi hili la ulipaji kodi wa Majengo. Kutoka kulia ni
Meneja Msaidizi Kanda ya Ilala kwa upande wa madeni Bw. Nuhu Ramadhani,
Meneja wa Kanda ya Ilala Bw. Abdul Mapembe na Bw. Revelian Kajuna.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto),
akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA)- Mbagala, alipotembelea ofisi hizo kujionea namna zoezi la ulipaji
kodi ya majengo unavyoendelea.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa katika
moja ya ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)- Mbagala na kukutana
na Mtoto Salma (aliyembeba) ambaye aliambatana na mama yake (hayuko
pichani) kwenda ofisini hapo kulipa kodi ya majengo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto)
akiongea na baadhi ya wazee waliojitokeza kulipa kodi za majengo katika
Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)- Mbagala jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto)
akiwapongeza vijana waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) - Mbagala jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment