Monday 16 June 2014

WORLD CUP 2014: GERMANY 4 - 0 PORTUGAL, THOMAS MULLER AFUNGA HAT-TRICK...PEPE ALIMWA RED CARD!

Germany V Portugal
 Thomas Muller Leo hii huko Arena Fonte Nova Jijini Salvador, Brazil, amepiga Bao 3 na kuisaidia Nchi yake kuizamisha kwa Bao 4-0 Portugal ambayo ilicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 37 baada ya Pepe kupewa Kadi Nyekundu.
Hii ilikuwa ni Mechi ya kwanza kwa Timu zote mbili ambazo zipo Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia pamoja na Ghana na USA ambao wanapambana baadae Usiku huu.
Muller alitangulia kufunga Bao lake la kwanza Dakika ya 12 kwa Penati iliyotolewa baada ya Mario Gotze kuangushwa na Joao Pereira.
Germany v PortugalMimi ndie Mwamuzi...............Haisaidii...!!! Ronaldo akilalamika kwa mwamuzi baada ya kunyimwa penati baada ya mchezaji wao kuangushwa kwenye eneo hatariGermany V PortugalKilichofata kwa Ujerumani ni kuongeza bao mbili tuu kipindi cha pili..
Mats Hummels alifunga Bao la Pili Dakika ya 32 na ndipo ikafuatia Kadi Nyekundu katika Dakika ya 37 kwa Pepe ambae alivaana na Muller na Refa kuamua ni Frikiki na yeye kumzonga Mjerumani huyo aliekuwa kakaa chini na kuinamisha kichwa chake kwake kumgusa Mullar kitendo ambacho Refa Milorad Mazic wa Serbia alichukulia kama fujo.
Kabla Haftaimu, Muller tena akapiga Bao na kuifanya Germany 3 Portugal 0.
Kipindi cha Pili, Thomas Muller akaongeza Bao lake la 3 Dakika ya 78 na Germany kushinda Bao 4-0.
Mechi inayofuata kwa Germany ni Jumamosi Juni 21 na Ghana na Portugal kucheza na USA Jumapili Juni 22.
Germany V PortugalNje!!! umejitafutia mwenyewe!!! umeskia tumekuja vitani!!Germany V Portugal Pepe akijitafuta mabaya!!!Germany V PortugalHatukuja kutalii hapa Brazil....hacha tushangilie........Germany V PortugalHummels akitupia bao la pili na kufanya 2-0Germany V PortugalThomas Muller akifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati usiku huu na kuitanguliza Nchi yake kwa bao 1-0 dhidi ya PortugalGermany V PortugalMashabiki wa Ujerumani wakitokelezea....tayari kupata alama tatu muhimu usiku huu...

No comments:

Post a Comment