Sunday, 22 March 2015

KAGASHEKI AZUNGUMZA NA WAAJIRI WAKE,MAELFU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA,AWATAKA WATENDAJI SERIKALINI KUWAJARI WANANCHI.


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki  katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru plat form  Bukoba amewataka watendaji ndani ya serikali katika maeneo tofauti kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao bila vitisho na matusi.Balozi Kagasheki ameseme unapofika wakati wa uchaguzi viongozi wa kisiasa wanakuwa na wakati mgumu kwa wananchi kwa ajiri ya baadhi ya watendaji wachache wanaonyanyasa wananchi katika matatizo mbalimbali, kitu kinachopelekea wananchi wengi kuwa na hasira na serikali yao inayoongozwa na chama cha Mapinduzi, Kitu ambacho amesema  hakuna kiongozi wa chama anaetoa huduma katika ofisi za serikali, na kibaya zaidi baadhi ya watendaji wamekuwa na kauli mbaya kwa wananchi kwa kusema kuwa  Si serikali ya ccm, kitu ambacho kinajenga chuki wananchi na chama.Pia ameongerea michango mingi inayobuka na hasa mashuleni na kusababisha kero kubwa kwa wazazi,Kwa upande wa wafanyabiashara  amezungumzia kero iliyokuwepo ya Tozo ya Ushuru ambayoiriwekwa na sheria ndogondogo  iliyopitishwa na Manispaa na kuonekana utaratibu unaotumika kudai hiyo pesa uangaliwe upya na kwa utaratibu ambao hautareta kero kwa wafanyabiashara, kwa maana ya mfumo unaotumika sasa wa kuweka viwango vikubwa.
 Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakimsikiliza Mbunge.
 Bwa Rugambwa  kwa raha zake.
 Wanasema vijana wa mjini Nyomi ya watu walifurika.
 Ukafika wakati wa kuchangia wasanii waliotoa albam ya nyimbo tatu kwa ajiri ya Mshikamano kwa wanaBukoba.
 Wamama wakipata raha ya Taarabu.
 Mh Mbunge akiwasiliri katika uwanja akipokelewa.
 Mwenyekiti wa CCM Bukoba Mjini Yusuf Ngaiza akimkaribisha Mbunge.
 Katibu mwenezi wa ccm Bukoba Mjini Ramadhani Kambuga akiendesha ratiba.
 Kulia ni Katibu wa ccm Bukoba Mjini.
 Mwenyekiti wa bodi maji Buwasa samora Lyakulwa (kulia) akiwa na Katibu msaidizi wa ccm mkoa.
 Kamanda wa vijana UVCCM Bukoba mjini Phirbert Nyerere akiongea na wananchi.

 Vijana katika hamasa.
 Kaimu mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Ngalinda.
 Mwenezi wa Mkoa wa Kagera akiongea na wananchi.
 Katibu wa Mkoa ccm akiongea na wananchi.
 Bw Muganyizi.
 Wasanii waliozindua albam maalumu kwa ajiri ya mshikamano Bukoba.
 Mwenyekiti ccm Bukoba mjini Yusuf Ngaiza akizungumza na wananchi.
 Mh Mbunge akiongea na wananchi, akuzungumzi swala la hali ya usalama katika jimbo,na hasa mauaji ambayo yamekuwa yakitokea na swala la kuchoma makanisa, amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la police kuwabaini wote wanahusika na mauaji ,kwa upande wa kuchoma makani ,Mbunge amesema  ni kitu kipya kimezuka kwa ajiri ya makusudio  fulani, lakini vyombo vya usalama wanashughulika nalo.
 Uzinduzi wa albamu ya mshikamano,mh Mbunge amewachangia milioni moja  ili ziwasaidie katika mahitaji yao.
 Bw Muganyizi akiwachangia vijana katika uzinduzi wa albamu yao.
 A lamin nae akawachangia vijana waliozindua albam yao.
Hakika ulikuwa ni mkutano mkubwa,na mwisho kabisa Balozi Kagasheki akasema yuko uwanjani katika kugombea ubunge na wananchi wasiwe na wasiwasi Bukoba ni ileile, watu ni walewale, nguvu ni ileile, na Kagasheki ni yuleyule kwa hiyo hana shaka.

No comments:

Post a Comment