Sunday, 31 January 2016

MAJANGILI YAUA RUBANI BAADA YA KUTUNGUA KWA RISASI NDEGE YA TANAPA



RUBANI wa helikopta ya Doria ya Mamlaka ya Wanyamapori Nchini, (TANAPA), Roger Gower raia wa Uingereza ameuawa baada ya kupigwa risasi akiwa angani na watu wanaosadikiwa kuwa majangili kwenye pori la akiba maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu majira ya jioni Januari 30, 2016.
Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Simiyu, Jonathan Shana ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio, amesema, askari mmoja wa wanyamapori aliyekuwemo ndani ya helikopta hiyo amejeruhiwa.
“Helikopta hiyo haikudunguliwa, bali risasi ilimpata Rubani na hivyo akauawa na helikopta kupoteza mwelekeo na kuanguka.” Alifafanua Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Simiyu, Jonathan.
“Tutawasaka pori kwa pori, pango kwa pango, kijiji kwa kijiji hadi tuwatie mbaroni wahalifu hao. Tumeleta FFU wenye silaha za nkutosha, ili kutekeleza amri ya kamanda IGP, Kamanda DCI na RPC, ndio maana tuko hapa na silaha nzito.” Alisema Mkuu huyo wa upelelezi wa Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, walifika eneo la tukio na kushngazwa na tukio hilo ambapo waziri alisema, sasa wahalifu hawa wamefikia kiwango cha juu cha uhalifu hadi kuhujumu teknolojia ya kuhifadhi mazingira, kwa kuwashambulia watendaji wetu, Waziri alisema kwa huzuni na kuongeza kuwa Serikali haitavumilia uhalifu huo na kuahidi kuwasaka popote walipo.
Hili ni tukio la kwanza kwa majangili kutungua kushambulia helikiopta ikiwa angani na kusababisha kifo.
 Waziri Profesa Maghembe, akizungumza baada ya kufika kwenye eneo la tukio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi
 Waziri akionyeshwa sehemu risasi ilipopenya kwenye helikopta hiyo
Askari na maafisa wa serikali wakionyeshana sehemu helikopta hiyo ilipopigwa risasi na kuanguka baada ya rubani kuuawa

No comments:

Post a Comment