Wednesday 18 December 2013

MSANII WA BONGO FLEVA ANAYEISHI NCHINI ITALIA REMMY WILLIAMS ATUA NCHINI KWA MAPOKEZI MAKUBWA


Remmy Williams akiwa ameshikwa mkono na meneja wake wa Tanzania, Mcdennis Mgatha.


MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Remmy Williams, anayefanya shughuli zake nchini Italia jana ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi na wasanii wenzake hapa nchini.

Akizungumzia ujio wake mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, alisema kuwa anawapenda wasanii wote wa Tanzania wanavyofanya vema nchini na kazi zao nyingi zinavuka mipaka kwa ajili ya kujitangaza kimataifa.

Hata hivyo yeye amejitokeza kuupaisha muziki huo kwa kushirikiana na wasanii atakaochaguliwa kushirikiana nae.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo, meneja wake nchini Tanzania, Mcdennis Mgatha, amesema msanii huyo kaja nchini kwa ajili ya kufanya kolabo na wasanii hapa nchini hivyo wapenzi wa muziki wakae mkao wa kula kwani ana vitu vingi sana alivyowaandalia ikiwemo nyimbo mpya pamoja na kufanya shoo kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hizo.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Remmy Williams akiwa na maua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Italia.
 
 Remmy (kushoto) akiwa na meneja wake wa nchini Italia, Wactor Fizio, walipowasili nchini.
Remmy Williams (katikati) akilakiwa na baadhi ya warembo waliojitokeza kumpokea uwanjani.

No comments:

Post a Comment