Thursday 11 June 2015

LOWASSA KUWASILI BUKOBA JUMATATU 15-6-2015 KWA AJILI YA KUPATA WADHAMINI.

 Waziri mkuu mstaafu na mgombea urais 2015  Edward Lowassa atawasili katika Manispaa ya Bukoba 15-6-2015 siku ya Jumatatu kwa ajili ya kupata wadhamini,Kwa taarifa  ya uhakika kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu sana wa Mh Lowassa ameseme atawasili majira ya saa tatu kamili katika uwanja wa ndege wa Bukoba kwa ndege maalumu,na baada ya hapo msafara wake utaondoka kuelekea ofisi za chama cha mapinduzi Mkoa wa Kagera na kukutana na wadhamini,Chanzo cha habari hii kimesema  hakuna kikomo cha wadhamini yeyote atakaejisikia na kuwiwa kudhamini anakaribishwa, Mh Lowassa kila mahala alipokuwa anakwenda watu wamekuwa wakijitokeza kwa wingi na kuonyesha mapenzi makubwa sana,(MANENO YA CHANZO CHA HABARI HII.)Hivyo amewaomba wale wote watakaoona wako tayari kudhamini wafike ,maana safari ya matumaini imewadia.
SAFARI YA MATUMAINI IMEWADIA.

No comments:

Post a Comment