Monday, 8 June 2015

KINANA AKAGUA MIRADI,ANG'AKA NA WATENDAJI NA WANASIASA WABADHIRIFU WANAOWAIBIA WANANCHI.

Katibu mkuu wa ccm Taifa Abdulrahaman Kinana ametembelea miradi mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba ikiwa ni ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya ccm 2010 -2015,Pia amekutana na Halmashauri kuu ya ccm Manispaa kuwasikiliza na kujua kero mbalimbali za wananchi,Mh Kinana ametembelea uwanja wa ndege wa Bukoba uliokarabatiwa  kwa kiwango cha rami na kuangalia maendelea ya ujenzi wa jengo jipya la mapokezi, pia ametembelea mradi mkubwa wa maji unaoendelea katika jimbo zima la Bukoba,Mh kinana alifuatana na Bw Nape ametembelea vikundi mbalimbali vya vijana na akina mama kujionea namna wanavyoshughurika na miradi yao,Mh Katibu mkuu Taifa Abdulhamani Kinana akiwa katika uwanja wa Uhuru Plat Form akihutubia wananchi amesema ,Chama kipindi cha uchaguzi ndio kinatafuta dora, na baada ya hapo inaundwa serikali,ila anasikitika kuona watendaji ambao hawajui hata serikali imepatikanaje wanakuwa wajeuri na kunyanyasa wananchi kwa lugha mbaya na kuwaibia,akasema ipo haja sasa ya kurekebisha baadhi ya sheria ambazo zimepitwa na wakati zinazolinda wabadhilifu wa mali za umma,akiongelea sakata la mradi wa viwanja elfu tano ,amesema anaomba wananchi wawe na subira limefika mahala pazuri na watafidiwa,maana ni kweli waliibiwa.

 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya ccm Bukoba Mjini wakiwa katika ukumbi wa St Francis.
 Bw Abdul Kagasheki Mnec Bukoba Mjini.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba .
 Kushoto , Mwenyekiti ccm  Bukoba Mjini Yusufu Ngaiza, Mwenyekiti ccm Mkoa Kagera Constancia Buhiye, Mbunge Balozi Khamis sued Kagasheki.
 Vijana Wamachinga Mh Kinana alifungua Saccos yao.
 Ni eneo la soko kuu Bukoba Mh Kinana alitembelea.

 Meneja wa uwanja wa ndege Bukoba akitoa taarifa.
 Muonekano wa jengo jipya la mapokezi la uwanja wa ndege Bukoba.
 Mh Kinana akiangalia maeneo mbalimbali uwanja wa ndege Bukoba.
 Alitembelea umoja wa akina mama wa Kastamu.
 Mradi wa maji.
 Mh Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa mradi mkubwa wa maji unaoendelea Bukoba.
 Mbunge akielezea mradi wa maji.
 Maelezo ya kina yakatakiwa maana muda wa makabidhiano umepita.
 Maagizo makali yakatolewa kukabidhi mradi.
 Mwenyekiti wa vijana mkoa Kagera Yahaya Kateme(kushoto) akiwa na bw Haridi.

Waendesha pikipiki wakiusindikiza msafara wa Kinana.

No comments:

Post a Comment