Thursday 20 February 2014

JIJINI DAR LEO BAADA YA RASHARASHA ZA MVUA


 Gari aina ya Isuzu likiwa limeanguka kwenye mtaro pembezoni mwa barabara ya Makongo eneo la Lugalo, haikuweza kufahamika kwa haraka chanzo cha ajali hiyo, lakini kubwa ikiwa ni utelezi katika eneo hilo kutokana na mvua za rasharasha zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam hii leo.  
 Wahusika wa gari hilo wakijadiliana jinsi ya kulikwamua gari hilo........
 Hapa ni eneo la Posta mpya barabara inayotoka Hidary Plaza, ikiwa imeharibika vibaya na kuwa na madimbwi yaliyofunikwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha baadhi ya madereva wa magari wasiojua ramani ya barabara hiyo, kukwama kama linavyoonekana gari hili likiwa limekwama katika eneo hili. 
 Eneo hili lilipokwama gari hili kuna shimo kubwa lililowazi.......
 Kuku wa Kisasa wakiwa katika usafiri wa Pick up kuelekea Soko la Kisutu tayari kwa kuuzwa kwa wateja. Pembeni mwa gari hilo ni askari wa usalama barabarani wakidili na waendesha bodaboda wanaokatisha njia hiyo kwa kuvunja sheria za usalama barabarani.
Hili ni eneo la Jangwani walipohamishwa wananchi waliopelekwa Mabwe Pande likiwa limebaki dampo la chupa chakavu na huku baadhi ya wananchi wakionekana kuendelea kuishi eneo hilo katika vibanda.

No comments:

Post a Comment