Sunday 16 February 2014

BALOZI KAGASHEKI AKUTANA NA MACHINGA WA BUKOBA MANISPAA,AWATAKA VIONGOZI WALIOPEWA DHAMANA YA KUONGOZA WANANCHI WASIWE WEPESI WA KUJIBU MAJIBU MEPESE KATIKA MAMBO YA MSINGI YANAYOHUSU MAISHA YA WATU

 Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini amekutana na wafanyabiashara ndogondogo(Machinga) wa Manispaa ya Bukoba baada ya kupeleka kilio chao katika ofisi za chama cha mapinduzi  Bukoba kutakiwa na uongozi wa Manispaa ya Bukoba kutoka katika maeneo wanayofanyia biashara zao. Balozi Kagasheki akijibu risara yao iliyokuwa imesheheni buguza na adha wanayopata kutoka kwa mgambo na katibu Tarafa amesema ni vizuri viongozi waliopewa dhamana   ya kuongoza na kushughulikia matatizo ya wananchi wawe makini na waache tabia ya kuwa wanatoa majibu mepesi kwa vitu  vinavyohitaji ufumbuzi wa tatizo, Mapema katika risara iliyosomwa na mwenyekiti wa umoja huo wa wamachinga walieleza na kuonyesha cheti cha usajili na kutambuliwa na manispaa ya Bukoba.,Balozi Kagasheki ndio akahoji unawezaje kirahisi kabisa kufukuza watu unaowatambua kisheria bila kuwatafutia eneo mbadala la kufanyia kazi,amewahaidi kulifanyia kazi na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao, Amewasihi na kuwaomba kuwa watulivu na wasikivu wakati swala lao likifanyiwa kazi, amewachangia kiasi cha shilingi milioni kumi ili zitunishe mfuko wao na kuwahaaidi kuwaongezea mtaji zaidi kama watakuwa waaminifu katika kukopeshana na kurudisha katika umoja wao.
 Mwenyekiti wa ccm Bukoba mjini  Yusuf Ngaiza akieleza jinsi chama kilivyopokea malalamiko yao na sasa wanamkabidhi swala hilo mh mbunge alishughulikie
 Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo akisoma risala kwa Mh mbunge
 Wafanyabiashara wakimsikiliza mh Kagasheki katika uwanja wa kaitaba Bukoba.
Mh diwani Felician Bigambo kata ya Bakoba (CUF) akimsikiliza Mh Kagasheki

No comments:

Post a Comment