Ni picha ya pamoja ya wafanyakazi wa jumuia ya Kasibante Redio waliondaa mlo wa mchana kwa ajili ya watoto yatima na walemavu wa viungo zaidi ya watoto 300 wakiwa na mliki wa Redio hiyo Balozi Kagasheki ambae alikuwa mgeni rasmi siku ya Valentine
Watoto kutoka Mugeza mseto, walemavu wa ngozi na macho
Matron wa watoto Mugeza mseto akiwa na mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja mlemavu wa ngozi alieletwa na mama yake akiwa na umri wa miezi minne akamuacha shuleni hapo mpaka sasa mama huyo hakuwahi kurudi kumuona mtoto huyu , na hamjui mama yake , matroni huyu mtoto ndio anamtambua kama mama yake, mama wa mtoto huyu inasemekana anaishi Karangwe alimleta mtoto huyu kwa ajili ya kuokoa maisha yake asiuwawe,baada ya kumkabidhi ni miezi minane sasa hakuwahi kurudi .
Hawa ni watoto viziwi nao walishiriki mlo
Kikundi cha ngoma cha rugoloire kilitumbuiza watoto na wageni walioudhulia
Ni baadhi ya zawadi mbalimbali ambazo zimekusanywa na jumuia ya Kasibante Redio kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya watoto
Mcungaji James akiombea chakula
Mzee Rwangisa na mgeni rasmi wakipata chakula
Watoto wakipata chakula
Mtoto huyo ni mlemavu wa macho baada ya kushiba akapumzika kidogo
Mama na mwana
Mkurugenzi wa Kasibante Redio Richard Leo akitoa neno na madhumuni ya kuandaa mlo wa mchana na watoto yatima na walemavu,lakini pia alieleza kuwa utakuwa ni mwendelezo wa kila mwaka kusherekea valentaine kwa staili hii
Mdau Paschazia Barongo nae alishiriki
Mgeni rasmi Balozi Kagasheki akitoa neno la shukrani kwa wate waliochangia kwa hali na mali kuwakumbuka viumbe wa mwenyezi mungu wenye ulemavu wa viungo na watoto wanaoishi katika mazingira magumu,katoa wito kwa jamii nzima kuwajari na kusaidia watoto wenye mahitaji.
Bw Kabantega
Binti huyu hana mikono yake yote miwili, anakula kwa kutumia miguu
Cheza twist...
Chezeee Richard na Jane weweeee
Maka chiiiiniii Tofauuu
Kijana Bale
Picha ya pamoja
Balozi Kagasheki akiongea na watato wanaoishi katika mazingira magumu aliokutana nao nje ya jengo la Kasibante Redio wakati akiondoka eneo hilo
No comments:
Post a Comment