Thursday, 15 May 2014

CAMERA YETU KIJIJI CHA BUGANDIKA NYUMBANI KWA BWANA KAMUZORA,AKIWA NA MAMA YAKE MZAZI ALIESTAAFU UTUMISHI WA UMMA IDARA YA AFYA

 Bw Kamuzora akiwa na mama yake mzazi anaeishi hapo nyumbani baada ya kustaafu utumishi wa umma na maisha yanaendelea kama mjini kijijini Bugandika.
 Ni nyumbani kwa BwKamuzora kijijini Bugandika
 Ilikuwa ni furaha kukutana na mama yake mzazi aliestaafu utumishi wa umma na sasa anaishi kijijini raha mustarehee
 Mama anaonekana mwenye furaha, tabasamu, si rahisi  kuelewa kama ni mama mstaafu katika idara ya afya na sasa yuko kijijini anaendelea na maisha, tumekuwa  tukiwaona watu wengi wanapostaafu kazi  maisha yana badilika na kupoteza mwerekeo, na wengi hukataa kurudi vijijini na kukatalia mijini kwa sababu  ya kutojipanga, mama huyu ni mfano mzuri wa kuigwa
 Iliweza kutueleza maisha yake ya kila siku na kusema maisha ya hapo kijijini ni mazuri sana , maana kila anachohitaji anakipata, miundo mbinu ya umeme hipo, hivyo anaweza kuweka, kuifadhi vyakula kwenye Friji, anapata habari zote za dunia kwa kutumia Tv, hivyo maisha mazuri ambayo angepata akiwa mjini anayapata akiwa Bugandika
 Bw Bushira akiwa na mama
 Ni utamaduni wa kihaya unapofika nyumbani kwa mtu unakarbibishwa kwa  kupewa kahawa ya kutafuna(akamwani)
 Hii ni picha ya baba mzazi wa Kamuzora aliefariki kwenye ajari ya meli ya Mv Bukoba
 Ni eneo la shamba
 Watoto majirani waekurahi na camera yetu
 Maisha yanaendelea  kama mujiniiiii
 Swaiba wake anafika ghafla nyumbani kwake
 Furahaaaa
 Bw Denis akiwa na Bw Bushira
Ongera mama mstaafu kwa kujiandaa vizuri, ni mfano wa kuigwa na wengine

No comments:

Post a Comment