Wednesday 14 May 2014

MVUA ILIYONYESHA JIJINI DAR JANA ILIVYOWATESA MADEREVA WA BAJAJI MIKOCHENI


 Dereva wa Bajaji yenye namba za usajili T 920 CMC, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, akijaribu kuikwamua Bajaji yake katika dimbwi la Maji huku ndani akiwa na abiria baada ya kuzimika katikati ya Dimbwi hilo eneo la Mikocheni A, jijini Dar es Salaam, jana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Eneo hilo limeharibika vibaya na hasa kutokana na barabara hiyo iliuwa tayari imeanza kukarabatiwa kwa kushindiliwa kifusi cha udongo kwa ajili ya kuwekwa lami, lakini zoezi hilo imeelezwa kutoendelea tena kutokana na mmoja kati ya waliokuwa wakitia msukumo kutengenezwa kwa barabara hiyo kuhama eneo hilo na kufanya ujenzi huo kusimama na kuharibika hadi kusababisha ufumbufu kwa madereva watumiao njia hiyo.
 Dereva wa Bajaji akienelea kuikwamua Bajaji yake kuwanushuru abiria wake wasihadhirike katika dimbwi hilo.
 Hapa akifanikiwa kuikwamua huku mmoja kati ya abiria akipitia kidirishani na kuingia upande wa dereva ili kuongoza bajaji hiyo.
 Moja ya chemba ya maji machafu ikiwa imefurika na kutema maji nje yaliyosababisha kuharibika kwa eneo la barabara hiyo.
 Chemba zikizidi kuzibuka eneo hilo

No comments:

Post a Comment