Friday 12 July 2013

TIJARA KABENDERA AELEZA KWA UFUPI HISTORIA YA MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI RWANDA ALPHA RWERANGIRA

Alpha Rwerangira(kushoto) mwanamuziki aliepata umaarufu mkubwa katikashindano la TUSKER ALL STAR 2011 na (kulia) ni meneja wake TIJARA KABENDERA ambae anamatumaini makubwa na ndoto ya kufanya makubwa na ALPHA katika muziki Alpha aakiwa katika katika moja ya show(ALPHA BAND WITH FAMILIES SEASON) iliyoandaliwa na cocacola nchini rwanda   AlphaRwirangira ni kijana aliezaliwa na mama mtanzania na baba mnyarwanda alizaliwa mkoa wa Geita, mama yake mzazi anaitwa Zouliette Ibrahim  mzaliwa wa mkoa shinyanga Tanzania na baba yake ni Bizima Joseph ambae ni mnyarwanda alieishi mkoani kagera, bukoba mjini. Baadae alirudi Rwanda mnamo mwaka 1996,.Alpha ni mtoto wa kwanza ktk familia ya watoto watano..amesoma shule za msingi tofauti nchini Tanzania .kama mwenge pr school,uhuru pr school,alikwenda kumalizia masomo yake ya awali nchini kenya...alipomaliza shule ya msingi alienda Rwanda kujiunga na familia yake alipoendelea na masomo ya sec ktk shule ya APRED NDERA alisoma mpaka senia six...Alpha aiingia ktk muziki akiwa anaimba kwenye kwaya ya kanisa.Badae alijiunga  kwenye  mashindano ya kimataifa TPF3 na kuibuka mshindi. na hapo ndio.. maisha ktk muziki yalipoanza mpaka leo hii...baada ya kushinda TPF3 aliendelea kufanya muziki na cholabo na wasani tofauti tofauti  wa E A..kama baby cool wa Ug na akatoa kibao kilichopendwa sana na kujipatia tuzo ya BEST SONG OF THE YEAR ktk award zinaitwa PAM AWARD nchin UG... katika nyimbo yake inayoitwa SONGA MBELE akimshilikisha binamu yake wa damu(kwani ni mtoto wa shangazi yake) AMBWENE YESAYA (AY) baada ya hapo alichaguliwa kama msanii mzuri wa kiume wa mwaka EA baada ya hapo alishiriki TUSKER ALL STARS iliyofanyika mwaka 2011 na kuibuka mshindi,mbali na kushiriki matamasha mbalimbali mwaka 2010 Alpha alibahatika kushiriki kutoa burudani katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Rwanda ,na katika uchaguzi huo KAGAME alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo,kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya katika kampeni za rwanda rais KAGAME aliweza kumlipia gharama za masomo  nchini marekani.  mpaka sasa mwanamuziki huyu nguli na kipendezi cha mashabiki wengi nchini rwana na nchi zingine yupo marekani akisomea muziki na managment,masomo hayo atayamaliza baada ya muda si mrefu kwani atakuwa amemaliza miaka mitano tangu ayaanze ,japo kuwa yupo masomoni amekuwa akiendelea na shughuli za muziki chini ya meneja wake TIJARA KABENDELA SHINANI ambae ni mwandishi wa habari anaeishi rwanda ,TIJARA akiongea na jamcobukoba.blogspot.com amesema anaamini Alpha atakapokuwa amemaliza masomo yake atakuwa anauwezo mkubwa sana katika kuujua muziki na watafanya mambo makubwa zaidi katika muziki,kwa sasa  ALPHA ametoa nyimbo mpya akishirikiana na binti wa kimarekani  LAMIYA GOOD kibao kinachoitwa HEAVEN.
HIYO CHINI NI LINK YA KIBAO CHAKE KIPYA...HEAVEN

No comments:

Post a Comment