Monday 8 July 2013

ROTARY CLUB MZIZIMA YAPATA RAIS WAKE


Monday, July 8, 2013

ROTARY CLUB MZIZIMA YAPATA RAIS WAKE

 Rais mpya wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es Salaam, Rotarian Ambrose Nshala, akihutubia katika hafla ya kumsimika rais mpya wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Rais huyo amechaguliwa kwa mwaka wa pili kushika uongozi huo. Wengine kutoka kushoto ni Gavana Mstaafu, Amu Shah, Theodosia Muhulo ambaye ni mke wa rais huo na Gavana Msaidizi wa Rotary, Irene Kamau.
  Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es salaam, Rotarian Ambrose Nshala(kulia), akimvisha pini rotarian mpya, Mhandisi Dennis katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Rais wa klabu ya Rotary ya Mzizima Dar es Salaam, Rotarian Ambrose Nshala (kulia), akimpa nyaraka rotarian mpya wa klabu hiyo, Paul Mashauri katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.
 Rais mpya wa klabu ya Rotary ya Mzizima, Dar es Salaam, Rotarian Ambarose Nshala (kulia), akimvisha pini mmoja wa wajumbe wa bodi ya klabu ya Rotary ya Mzizima, Rotarian Edith Lyimo katika hafla hiyo
jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni wajumbe wa bodi hiyo, Emeria Mugonzibwa na Rotarian Ailinda Sawe.
 Rais wa Rotary klabu ya Mzizima, Rotarian Ambrose Nshala (kushoto) akiwaongoza wanachama wengine wa klabu hiyo kuselebuka katika hafla ya kmsimika rais na viongozi wengine wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanachama wa klabu ya Rotary ya Mzizima, Dar es Salaam wakijimwaga ukumbini katika hafla hiyo jijini humo mwishoni mwa wiki.
Wasanii wa kikundi cha Safi Theatre Group wakifanya vitu vyao  katika hafla ya kumsimika rais na viongozi wengine wa klabu ya Rotary ya Mzizima jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment