Wednesday, 10 July 2013

BALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELIGIJI DR DIODORUS B . KAMALA ASEMA KAMA, ANGEULIZWA UBALOZI NA UBUNGE ACHAGUE KIPI, YEYE ANGECHAGUA UBUNGE MAANA ANAKUWA KARIBU NA WANANCHI

 Balozi Diodorus Kamala akiwa katika mahojiano ya (LIVE) ambayo anasikika kila mahala kwa muda huo, akiongea na mwandishi wa habari wa redio karagwe akimuhoji mambo mbalimbali na ususani maswala ya wilaya ya misenye ambayo alisema kipindi akiwa mbunge wa jimbo la misenye aliweka jitihada kubwa sana ili misenye iweze kuwa wilaya, na katika hilo alifanikiwa na leo ni wilaya
 Akijibu swali la mwandishi kuhusu mbunge aliepo mh asumpta, amewaomba wananchi wote wa jimbo  la misenye kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuleta maendeleo, ili mwisho wa siku ukimuohoji katika kipindi chake cha uongozi alifanya nini isije ikaonekana hawakumpa ushirikiano.
 DR Kamala aliongerea pia swala la ajira ya vijana kwa kusema suluhisho si kuwakamata vijana eti ni wadhululaji, maana hakuna anaetoka nyumbani eti atembee ovyo,swala hapa ni viongozi kutatua tatizo na kupata suluhisho,akasema ndio maana yeye ameandaa kongamano kubwa litakalofanyika huko ulaya mapema mwezi wa kumi mwaka huu akishirikiana na nchi zingine kuzindua mpango wa kumsaidia kijana kupata ajira,balozi kamala  amesema umefika wakati  sasa umefika kijana aliehitimu fani fulani si kumpa tu cheti apewe cheti na vitendea kazi ili  apate ajira ya moja kwa moja. Balozi kamala (akiwa na jamal kalumuna mmiliki wa jamcobukoba.blogspot.com)
 Balozi Kamala akaulizwa kati ya ubunge na ubalozi kipi angechagua,akajibu kwangu ubunge ni bora kuliko ubalozi, maana ubunge unanipa fursa ya kuwa karibu na wanachi na kufanya kazi nao za maendeleo kwa karibu zaidi.(katika picha balozi kamala akiwa na Gulam visram ambae balozi anapokuwa bukoba muda wote anampeleka kwa gari anapohitaji kufika)
 Balozi kamala akiwasili uwanja wa ndege bukoba leo mchana kuelekea dar tayari kwa safari ya kurejea beligium
 Ndugu Basibira akiwa na balozi kamala sehemu ya mapokezi uwanja wa ndege bukoba,ndugu basibira mara nyingi utamkuta uwanja wa ndege wa bukoba kila ndege inapoondoka na kutua na hii inatokana na mahusiano yake mema na kuwa na mtandao mkubwa wa kufaamiana na watu, tunakupongeza kwa hilo mzee basibira.
 Balozi kamala akiwa chumba cha wageni wa VIP bukoba alikutana na ndugu Kenyera afisa mwandamizi wa jeshi la polisi na pembeni mwake ni afisa upelelezi wa mkoa wa kagera
                                      Balozi kamala akiwa na mwandishi wa habari redio karagwe
                            Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot kwa matukio ya muda wote

No comments:

Post a Comment