Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki akizungumza na wageni waalikwa
wakati wa uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya Mwaka 2013
ambayo imejikita kiundani zaidi kuangalia muunganiko wa Mahusiano ya
Kibiashara na Uwekezaji Duniani.
Bi. Kairuki amesema Tanzania imeweza
kupata Uwekezaji mara dufu katika maeneo ya Mafuta na Utafiti wa Gesi
Asilia katika kusukuma pato la taifa kuongeza ajira na kupambana na
umaskini.
Ameongeza Muunganiko wa Biashara na
uwekezaji umepata mwamko mkubwa sana kutoka kwenye makampuni makubwa
duniani na umeleta fursa kwa nchi maskini na zinazoendelea kama Tanzania
kuwa na uhusiano mzuri kiuchumi na nchi zilizoendelea. Uzinduzi huo
umefanyika leo jijini Dar kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirika la Kazi
Duniani (ILO).
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali na mabalozi wakifuatilia uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo ya Uwekezaji Duniani.
Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano
na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara
(UNCTAD) Manuela TORTORA akizungumzia umuhimu wa sera za nchi za
Uwekezaji kuhakikisha zinatoa fursa ya ajira na kupunguza umaskini
katika nchini zinazoendelea.
Viongozi wa taasisi mbalimbali, Mabalozi, Waandishi wa habari katika uzinduzi huo.
Mwezashaji katika uzinduzi wa Ripoti
ya Ywekezaji wa Kigeni Duniani ya Mwaka 2013 Stella Vuzo Afisa Habari wa
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akiwakaribisha
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki
na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara Manuela TORTORA kuzindua rasmi
ripoti hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi
Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya
Biashara Manuela TORTORA kwa pamoja wakizindua rasmi Ripoti ya Uwekezaji
Duniani ya Mwaka 2013 iliyobeba kauli mbiu Muunganiko wa Biashara na
Uwekezaji Duniani "Global Value Chains".
Sasa imezinduliwa rasmi nchini Tanzania.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la kuendeleza Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi akichangia mada
baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013.
Kutoka kushoto Meza kuu ni Mkurugenzi
wa Utafiti na Mifumo ya Teknolojia kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini
(TIC) John Kyaruzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini
(TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela
TORTORA.
Usia Nkhoma Ledama kutoka Kitengo cha
habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akigawa Ripoti ya Uwekezaji Duniani
ya Mwaka 2013 kwa wadau waliohudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mdau akipitia ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi nchini.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment