Friday 12 July 2013

KAGASHEKI CUP 2013: IJUGANYONDO 0 vs BAKOBA 11, AIBU YAIKUMBA TIMU YA IJUGANYONDO YACHAKAZWA BAO BILA HURUMA!!!

Bakoba wakicheza kwa kujiamini na kucheza mchezo wa kuwashtukizia wenzao Ujuganyondo leo kwenye Kagasheki Cup 2013, Uwanja wa Kaitaba wameishindilia jumla ya mabao 11-0 timu ya Kata ya Ijuganyondo bila kujitetea!!!
Mchezo huu mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Bakoba walikuwa mbele ya bao 6-0 dhidi ya kibonde Ijuganyondo. Kipindi cha pili Bakoba waliendeleza ubabe wao wa kuziona nyavu na kweza kufunga bao 5 na huku wakikosa mabao mengi na ya wazi.
Benchi la Timu ya Bakoba
Benchi la ufundi na viongozi wa Bakoba wakiendelea kuangalia timu yao ikimenyana na timu ya Ijuganyondo
Kocha wa Ijuganyondo hakuweza kukaa maana alikuwa na jukumu la kuwahamasisha wachezaji wake nao waweze kufika kwenye lango la wenzao japo hawakuweza kufurukuta hata kidogo hata kusogea eneo la kipa.
Mchezo uliopigwa saa nane kamili mchana na timu ya Bakoba ikaibuka kidedea kwa bao 11-0 na kujiwekea historia ya pekee tangu Kagasheki ianze, Na kumbuka hawa Ijuganyondo juzi walicheza na Kashai na kufungwa bao 4-0 hivyo timu hii unaweza ukajionea mwenyewe kwa lugha nyingine unaweza ukasema ni kibonde!!!, Kwa kukujuza zaidi nakumbuka kwa haraka timu iliyowahi kufungwa mabao 11-0 ni ya mwaka 2011 Septemba 2 wakati timu ya uholanzi ilipoifunga bao 11-0 timu ya San Marino, Robin Van Persie mchezaji wa United alipoifunga bao nne mwenye na leo hii kuna mchezaji wa Bakoba kafunga bao tano mwenyewe!!!
Wachezaji wa Bakoba wakiwatoka wachezaji wa Ijuganyondo na kwenda kufunga.
Mashabiki jukwaa kuu walikuwa wakishangilia vilivyo baada ya kuona Mabao yaingia bila shida ya kukabwa na huku timu ya Ijuganyondo ikionekana kuzidiwa kila kitu!!

Mashabiki wakishangilia jukwaa kuu
Wadau wakifatilia soka wengine wakiponda kibonde Iujuganyondo

Furaha ikatanda kwa Mwinyi kushoto hapa!!! akiwa na wachezaji wa akiba

Mashabiki wakiwa hawana hamu!!! wengine wakisikitika kwa kile kinachoendelea na wengine wakisikitika kuona Bakoba wanaendelea kukosa mabao kadhaa kwenye goli la Ijuganyondo!!!
Shabiki akipuliza Vuvuzela la asili kuashilia soka hapa!!

wakati wa mapumziko Bakoba wakipongezwa kwa kazi nzuri!
Kiongozi mwinyi akiwapongeza wachezaji wa Bakoba

Mashabiki

Patashika za hapa na pale kwenye goli la Ijuganyondo!

Kikosi cha Bakoba

Bakoba wakijiachia kwenye kamera

Baada ya mechi kuisha Bakoba wakipongezana na kuomba kwa kile walichokifanya uwanjani Kaitaba cha kuwazaba Ijuganyondo bao 11-0


Patashika mchezaji wa Ijuganyondo aliumia kichwani baada ya kukogana kichwa na mwenzake

Kipa wa Ijuganyondo hoi!!!

Hoi!!!!!!!!! kibano cha 11-0!!............hakunaga!

No comments:

Post a Comment