Mshambuliaji
wa Yanga, Mrisho Ngassa, akiruka kupiga mpira wa kichwa na kufunga bao
la kwanza katika dakika ya 13 kipindi cha kwanza. Katika mchezo huo wa
Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Komorozine ya Comorro,
uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 7-0.
Ngassa
alipachika mabao matatu kati ya saba katika dakika za 13, 64 na 68. Bao
la pili lilifungwa na Nadir Haroub, katika dakika ya 16, Didier
Kavumbagu, dakika ya 57 na 80 na Hamis Kiiza, akifunga katika dakika ya
59.
Goooo, bao la kwanza Ngassa akimgalagaza kipa wa Komorozine....
Goooooo, bao la pili likifungwa na Canavaro.
Wakishangilia moja kati ya mabao yao....
David Luhende, akiwania mpira na kipa wa Komorozine....
Mrisho Ngasa akishangilia bao lake la tatu....
Sehemu ya mashabiki
Ngasa akishangilia na Oscar Joshua.....
Wakomorozine hoi baada ya kipigo hicho.....
Ubao wa matangazo unavyosomeka hadi mwisho wa mchezo huo.
Makocha wakipongezana baada ya mchezo huo....
Mbuyu Twite akichezewa faulo.....
Hamis Kiiza akiwania mpira na beki wa Komorozine....
Haruna Niyonzima, akimfanya kitu mbaya beki wa Komorozine....
*YANGA INAONGOZA MABAO 2-0 UWANJA WA TAIFA DHIDI YA KOMOROZINE
Nahodha
wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akijikunja kupiga mpira wa
kichwa cha chini na kufunga bao la pili, baada ya mpira wa adhabu
uliopigwa na David Luhende baada ya Mbuyu Twite, kuchezewa Faulo na beki
wa Komorozine, Ali Mohamed. Bao la kwanza lilifungwa na Mrisho Ngasa,
akiunganisha mpira wa Krosi iliyopigwa na Simon Msuva.
Mshambuliaji
wa Yanga, Hamis Kiiza, akijaribu kuuwahi mpira mbele ya beki wa
Komorozine, wakati wa mchezo huo kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa Yanga, wakicheza kushangilia bao la kwanza lililofungwa na Mrisho Ngasa (katikati).
*WANAOANZA KUWAKIMBIZA WAKOMORO UWANJA WA TAIFA MUDA HUU
Kocha wa Makipa Juma Pondamali, akiwafua makipa Deogratius Munishi na Juma Kaseja, wakati wa kupasha misuri moto.
Timu zote hivi sasa zinaingia uwanjani tayari kabisa kwa kukaguliwa kuanza mtanange huo.
VIKOSI VINAVYOANZA
YANGA:- Juma
Kaseja, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub (c), Kelvin Yondani,
Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Hamis Kiiza, Mrisho Ngassa
na David Luhende.
RIZEVU:- Deogratius Munishi, Rajab Zahir, Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Juma Abdul, Hussein Javu, na Hassan Dilunga.
WACOMORO:-
Attoumani Farid, Ali Mohamed, Nizar Amir, Abdou Moussoidikou, Ahamadi
Houmadi Anli, Moidjie Ali, Mortadhoi Fayssoil, Attoumane Omar, Mohamed
Erfeda (c), Mouayade Almansoor na Ahmed Waladi.
Wachezaji wa Yanga wakiingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kupasha misuri
Wachezaji wa Comorro, wakiingia vyumbani....
Sehemu ya mashabiki.
No comments:
Post a Comment