Friday 7 February 2014

BREAKING NEWS...MTU ALIETAMBULIWA KWA JINA BAHATI AKUTWA KAJINYONGA UFUKWE WA SPICE MOTEL BEACH HIVI PUNDE.

 Mtu mmoja alietambulika kwa jina moja la Bahati maarufu kwa uuzaji wa mifuko ya plastiki maeneo ya stand kuu ya mabasi Bukoba amekutwa kajinyonga juu ya mti kama unavyoona maeneo ya ufukwe wa Spice Motel majira ya saa nane mchana huu, Taarifa za awali  kutoka kwa watu waliokuwa katika tukio hilo wanasema , kabla ya kifo cha marehemu walipita eneo hilo marehemu alionekana akiwa na mafurushi ya vitu na alikuwa akifua katika eneo hilo la ufukwe,Mtu mmoja ambae hakuwa tayari kutaja jina lake amesema leo majira ya saa 12.00asubuhi amesalimiana na marehemu maeneo ya stand ya mabasi akiendelea na shughuli yake ya kutembeza mifuko ya plastiki kwenye mabasi yanayokwenda  mikoani na maeneo mengine akiwa mzima wa afya.Mwili wa marehemu umepelekwa Hospital ya Mkoa  wa Kagera kuifadhiwa kwa ajili ya kutambua ndugu wa marehemu.
 Askari akiwa amepanda mti ili aweze kukata kamba aliyotumia kujinyonga
 Amekutwa katika hali hii
 Haijafahamika ni wa nini kachukua maamuzi haya
 Mwili wa marehemu ukishushwa
 Kamanda wa polisi wilaya ya Bukoba akishuhudia tukio
 Wananchi waliokusanyika katika tukio
 Mkuu wa kituo cha polisi Bukoba(mwenye koti) akiwa anaangalia baadhi uya vitu vya marehemu alivyokuja navyo kabla ya kujinyonga
 Hivi ni vitu vya marehemu alivyokuja navyo babla ya kujinyonga
 Maeneo ya spice beach
 Mmoja wa watu wa kwanza kutoa taarifa kituo cha polisi Mma Faima
 Mwili wa marehemu ukipakiwa kwenye gari la polisi
Mwili wa marehemu ukipelekwa kuifadhiwa hospital ya mkoa wa kagera

No comments:

Post a Comment