Agizo hilo limetolewa hivi karibuni katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Iringa kilichofanyika katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo chini ya mkuu wa mkoa huo, Christine Ishengoma.
Hayo yamekuja baada ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi kuwaeleza wajumbe kuwa mbali ya kusikia kutoka majiji kama Dar na mengine nchini kwamba biashara za ukahaba na ushoga ziko juu, uchunguzi unaonesha mji wa Iringa ni miongoni mwa miji ambayo biashara hiyo inaendelea kukua kwa kasi.
“Ndugu wajumbe, Manispaa ya Iringa ina watu wanaofanya biashara ya ushoga na ukahaba. Mimi meya nina ushahidi wa kutosha. Idara inayohusika na vita dhidi ya Ukimwi katika halmashauri ya manispaa inaujua mtandao mzima wa biashara hiyo haramu,” alisema meya huyo.
Kufuatia ushahidi huo kutoka kwa meya, mkuu huyo wa mkoa alilazimika kusimama na kuwataka wahusika kuwakamata watu hao wote ili ikibidi wasaidiwe kupewa miradi rafiki badala ya kuendelea na biashara hiyo haramu.
No comments:
Post a Comment