Polisi
wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya wakifungua dawa
zilizokamatwa jana kwenye jahazi liitwalo Kunarak-Iran lililokutwa
katika Bahari ya Hindi eneo la Tanzania likiwa na kilo 201 za heroini,
pamoja na raia wanane wa Iran na Wapakistan wanne.
Kikosi
kazi cha Jeshi la Polisi cha Kudhibiti Uharamia Baharini kimekamata
kilo 201 za dawa za kulevya aina heroini zilizokuwa zikiingizwa nchini
kutoka Iran.
Kamishna
wa Polisi, Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa,
alisema jana kikosi hicho kikiwa kwenye doria ya kawaida kiliona boti
ambayo haikuwa na bendera wala kiashiria chochote ndipo walipoitilia
shaka na kuamua kuifuatilia.
Nzowa
alisema kuwa mzigo huo ni mkubwa zaidi wa heroin kuwahi kukamatwa na
vikosi vya doria vya Tanzania. Alisema mara ya mwisho kwa mzigo mkubwa
zaidi wa heroin kuwahi kukamatwa ilikuwa mwaka 2012 wakati zilipokamatwa
kilo 70 za dawa hizo jijini Dar es Salaam.
Nzowa
alisema Kikosi cha Wanamaji kiliposhuku boti hiyo, kiliisimamisha na
kugundua kuwa ilikuwa na watu 12. Alisema baada ya uchunguzi wao
waligundua kuwa kulikuwa na raia wanane wa Iran na wanne wa
Pakistan. “Boti hiyo ilivutwa hadi ufukweni ambako leo (jana) ilifanyiwa
uchunguzi na ndipo zikakutwa na kilo 201 za heroin,” alisema Nzowa.
Nzowa
alisema boti hiyo iliyosajiliwa Kunarak, Iran, ilikuwa inaongozwa na
nahodha mwenye uraia wa nchi hiyo, Ayub Hot (50). Nzowa alisema
kitakachofuata sasa ni kufanya upelelezi na kujua walikuwa wanataka
kupeleka wapi mzigo huo, kufahamu mtandao wao na walipanga kufanya nini
katika ufukwe wa Dar es Salaam. Alisema baada ya upelelezi wao kukamilika watu hao watafikishwa mahakamani. Naye
Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Polisi, ACP Mboje Kanga alisema watu
hao 12 hivi sasa wamewekwa mahabusu ya wanamaji na kikosi hicho kwa
kushirikiana na Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya wataendelea na
upelelezi.
No comments:
Post a Comment