Wednesday 15 May 2013

NAY WA MITEGO, DIAMOND PLATINUMZ NDANI YA JUKWAA MOJA "DAR lIVE" MEI 18.2013


WASANII wa Muziki wa Kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' na Ney wa Mitego wanatarajia kupanda jukwaa moja kumtafuta nani mkali katika uzinduzi wa video ya ‘Muziki Gani’ itakayozinduliwa Mei 18 katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi wa video hiyo ambao umeandaliwa na Kampuni ya Yuneda Entertainment itawapambanisha wasanii hao kutafuta nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva.
Wimbo ‘Muziki Gani’ unakwenda kwa staili ya kubishana kati ya aina hizo za muziki.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kutambulisha uzinduzi huo, Mratibu wa onesho hilo Kahabi Mwendesha alisema utapambwa na wasanii wa Hip Hop na Bongo Fleva na kuwataka mashabiki wafike kwa wingi ili kushuhudia wababe hao.

Alisema baada ya video hiyo kuzinduliwa Dar Live, uzinduzi huo utahahamia mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza na baadaye Arusha na amewataka mashabiki kukaa tayari kwa burudani hiyo.
Alitaja kiingilio katika onesho hilo ni sh 10,000 huku akisisitiza kuwa kutakuwa na ulinzi imara na kuwataka wapenzi na mashabiki wa Simba na Yanga, wafike ukumbini siku hiyo kwani mechi baina ya timu hizo itaoneshwa ‘live’.
Bw. Kahabi akifanya Press ya uzinduzi wa VIDEO ya Muziki Gani ya Nay wa Mitego ft Diamond ambayo itafanyika jumamosi hii Ndani ya ukumbi wa DARLIVE tarehe 18.05.2013.

No comments:

Post a Comment