Tuesday 14 May 2013

CAMERA YETU BARABARA YA ARUSHA MANISPAA YA BUKOBA

Takribani miaka ya 2010-2012 barabara ya arusha ilikuwa maarufu kwa vibanda vya wauza kuku na maduka ya spea za baiskeli,Lakini ghafla mwishoni mwa mwaka 2012 kasi ya mabadiriko ya maduka na shughuli za kibiashara kushamili kwa muda mfupi na barabara hiyo kuonekana muda mwingi kuwa na msongamano wa watu na magari. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za biashara hatukusita kuhoji baadhi ya wafanyabiashara ambao tumewakuta katika maeneo ambayo hapo siku za nyuma yalikuwa na makazi ya watu kuishi lakini sasa yanatumika kwa shughuli za kibiashara,mfanyabiashara mmoja aliejitambulisha kwa jina Miraji hussen alisema mapema mwezi wa kwanza mwaka huu 2013 wafanyabiashara wengi waliomo soko kuu bukoba walikuwa watoke kwa ajili ya ujenzi wa soko,hivyo wengi wao walifanya jitihada binafisi kutafuta maeneo ya kuamishia shughuli zao,ndo maana kwa ajili hiyo nyumba nyingi zilizokuwa maeneo ya barabara ya arusha wamiliki walizibadilisha na kuwa za biashara kwa hiyo ndio sababu kubwa ya mabadiliko, japo tunasikia kuwa mpango wa uvunjaji wa soko umesitishwa mpaka hapo badae,miraji husseni alisema.

Mitaa hii watu huja kutengeneza pikipiki na kunywa kahawa



Dada Lucy akiwa saloon,barabara ya Arusha




Duka la spea za baiskeli kwa ngugu Miraji Hussein

Ndugu Ramadhani anauza vifaa vya umeme

Kitambo dada huyu anafanya biashara barabara hii ya Arusha


Barabara ya Arusha hiko busy muda wote





Vibanda vya wauza kuku,hapa ndio soko kuu kwa bukoba ukihitaji kuku



Kitambo nyumba ya wageni ipo mitaa hii,wengi wenu mmepita hapa


Dada Jovensi ni mmoja wa waanzilishi wa maduka katika barabara ya Arusha

Amir Hamza ni wakala wa kusambaza sukari kutoka katika kiwanda cha sukari kagera,huduma hii imechangia kwa kiasi kikubwa barabara ya Arusha kuwa na msongamano wa magari wakati wakipakia sukari

ndugu Mwinyi akiwa kazini





Miaka ya 2011 katika barabara ya Arusha lilikuwepo duka la ndugu Abasi tu, leo yapo kibao

Maduka ya nguo za kike na kiume yapo mengi sana maeneo hayo





Nilikutana na huyu dada barabara ya Arusha nikiendelea na kazi, mtaa huko busy na magari saa zote



maeneo yote haya ya maduka,saloo yalikuwa makazi ya watu barabara ya Arusha





Manywele design duka jipya ,mwanzoni ilikuwa nyumba ya kuishi sasa ni duka





Takribani yapo maduka matano kwenye kwenye jengo hili, ni nyumba mama nyamwihura ilikuwa nyumba ya kuishi sasa ni maduka, barabara ya Arusha

No comments:

Post a Comment